Wema Sepetu ajifananisha na dhahabu.....MTAZAME AKIKATA MAUNO.

Wema  Sepetu
MREMBO wa filamu Tanzania, Wema  Sepetu, amesema yeye ni dhahabu inayogombewa na watu hivyo hajali hata kama atachafuliwa namna gani katika mitandao ya kijamii.
Wema alisema kwamba, hana mpango wa kujibu vibaya vinavyoongelewa kuhusu yeye kwa kuwa yeye bado ni dhahabu inayotamaniwa kushikwa na kila mtu.
“Mimi ni kama dhahabu hivyo kila mtu anatamani kuishika, watu wanaacha kufanya yao kila siku Wema,  kwa sasa niko na mambo yangu ya kutafuta fedha sina habari na mtu hata aniandike vibaya vipi,” alisema Wema.
Aliongeza kwamba licha ya kusemwa, amezidi kujiongezea mashabiki na mikataba mbalimbali ya kufanya kazi na makampuni yenye majina makubwa kwa kuwa yeye ni kama dhahabu isiyochafuka.
MTAZAME HAPA AKIKATA MAUNO.....
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment