Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na
Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli, leo tarehe 25 Desemba, 2016 wameungana
na waumini wa Jimbo Katoliki la Singida kusali Misa ya Krismasi
iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatatifu wa Yesu Mjini
Singida.Misa hiyo Takatifu ya Krismasi imeongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida Mhashamu Edward Mapunda.
Akizungumza
mara baada ya kumalizika kwa Misa Takatifu, Mhe. Rais Magufuli
amewatakia heri ya Krismasi waumini wote wa Jimbo la Singida na
Watanzania wote kwa ujumla na amewasihi kusherehekea kuzaliwa kwa Bwana
Yesu kwa kuendeleza amani na upendo na kuacha vitendo vya kubaguana kwa
misingi ya dini, kabila, itikadi na kanda zao.
Dkt. Magufuli
amewahimiza Watanzania wote kuongeza juhudi katika kuchapa kazi kama
alivyofanya Bwana Yesu na pia amesema kwa kuwa maeneo mengi ya nchi
yameonekana kukabiliwa na uhaba wa mvua, ni vema wakatumia vizuri mvua
chache zinazoendelea kunyesha kuzalisha mazao yanayokomaa haraka ili
kuepuka upungufu wa chakula.
Kwa upande wa Mkoa wa Singida ambao
ni maarufu kwa kilimo cha alizeti, Mhe. Rais Magufuli amewasisitiza
kuchangamkia fursa ya ujenzi wa viwanda ambayo nchi inatoa kipaumbele
kwa kuzalisha alizeti kwa wingi ili zitumike kuzalisha mafuta ya kupikia
kwa wingi.
Jaffar Haniu Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Singida 25 Desemba, 2016
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Blogger Comment