Kamanda wa Mkoa wa Tabora, Khamis Issah Sulemani.
WATU wawili waliokuwa wamejeruhiwa kwa risasi wakati wa mapambano na majambazi katika kijiji cha Isila, wilaya ya Uyui mkoa Tabora, wamefariki dunia wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora.
Tukio hilo ambalo lilitokea usiku wa kuamkia juzi ambapo majambazi watatu wakiwa na bunduki aina ya SMG, walivamia nyumbani kwa mfanyabiashara wa ng’ombe na kuwajeruhiwa kwa risasi watu wawili huku jambazi mmoja akiuawa wakati wa majibizano ya risasi na polisi na wengine wawili kutokomea kusikojulikana.
Akithibitisha kutokea kwa vifo hivyo vya Bw. Mirija Bapa na ndugu yake Umoja Ubapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Khamis Selemani amesema kuwa watu hao walizidiwa ghafla wakati wakipata matibabu na kupeleka vifo vyao.
Blogger Comment