Shahidi kesi ya kutakatisha bil 7/-augua ghafla

Mfanyabiashara Anayedaiwa Kujipatia Milioni 7 Kwa Dakika Afikishwa Mahakamani Na Kusomewa Mashitaka 199KESI ya wizi ya Sh bilioni saba inayowakabili waliokuwa wafanyakazi 13 wa Benki ya Exim Arusha imeahirishwa baada ya shahidi wa nane katika kesi hiyo kuugua.
Akiomba kuahirisha kesi hiyo jana mbele ya Hakimu Mfawidhi ya Mahakama ya Wilaya ya Arusha/Arumeru, John Kamugisha, Mwanasheria wa Serikali Paul Kaduchi alisema shahidi aliyepaswa kutoa ushahidi ameugua ghafla, hivyo kuiomba mahakama yako iahirishe kesi hiyo hadi siku nyingine.
“Naiomba mahakama yako tukufu iahirishe kesi hii kwa sababu hiyo ambayo imetokea ghafla na sio lengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuahirisha kesi hii leo,” alisema Kaduchi.
Baada ya ombi hilo, Hakimu Kamugisha aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 27, mwaka huu itakapotajwa na kuanza kusikilizwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 2, mwaka huu na aliagiza kuwepo kwa mashahidi siku hiyo bila ya kukosa.
Katika kesi hiyo, waliokuwa wafanyakazi wa Benki ya Exim wanatuhumiwa kutakatisha fedha zaidi ya Sh bilioni saba kwa kutumia mfumo wa kibenki wa kielektroniki katika kipindi cha mwaka 2011 hadi 2012 kwa nyakati tofauti.
Katika kesi hiyo aliyekuwa mfanyakazi benki hiyo, Neema Kinabo (30) alikiri kosa na kulipa faini ya Sh milioni 130 na kuachiwa, na mwingine mfanyabiashara Mosses Chacha (37) naye alikiri kosa na kulipa faini ya Sh milioni 100 na wote waliachiwa huru kwa nyakati tofauti.
Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Kesi ya Utakatishaji Fedha, hukumu yake kisheria ni kati ya miaka mitano hadi 10 au faini ya kiwango cha chini Sh milioni 100 na haizidi Sh milioni 500.
Wafanyakazi hao ni pamoja na aliyekuwa Meneja wa Exim Arusha, Bimel Gondalia (37) anayatetewa na wakili Adamu Jabir, Lilian Mgaya (33) anatetewa na mawakili wawili Arnold Laizer na Philipo Mushi, mshitakiwa wa nne Livingstone Julius (36) anatetewa na wakili Mosses Mahuna.
Mshitakiwa wa tano, Joyce Kimaro (36) anatetewa na wakili Laizer na Mushi, mshitakiwa wa sita Daud Mosha anatetewa na wakili J. Mjema, mshitakiwa wa saba Doroth Tigana (50) anatetewa na wakili Edna Haraka, mshitakiwa wa nane, Evans Kashebo (40) hana wakili, mshitakiwa wa 10, Tuntufe Aggrey (32) anatetewa na wakili Fediles Peter.
Mshitakiwa wa 11, Joseph Meck (34) hana wakili na mshitakiwa wa 12, Janes Massawe (32) anatetewa na mawakili Laizer na Mushi, wakati mshitakiwa wa 13, Christopher Lyimo (34) anatetewa na wakili Laizer na Mushi, mshitakiwa wa 14, Gervas Gugo ambaye si mfanyakazi wa Exim, anatetewa na Laizer na Mushi na wa 15, Deodet Chacha (35) anatetwa na wakili N. Wantora.
Washitakiwa wanne ambao ni Gomes, Kashebo, Meck na Lyimo wako nje kwa dhamana. Washitakiwa wengine wote wako rumande kwa kudaiwa kutakatisha fedha. Kwa mujibu wa sheria kesi hiyo haina dhamana.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment