Linah Sanga Ahofia Kuweka Wazi Uhusiano Wake wa Mapenzi

Linah Sanga
Linah amesema hayupo tayari kuweka mahusiano yake wazi kwa sasa.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha E-News cha EATV kuwa wapo watu kwenye mahusiano wanataka kujaribu penzi la mtu kwa kumchezea na hawana mipango yoyote ya baadaye.

Linah ameongeza kuwa kwa sasa yeye hayupo tayari kumweka wazi mpenzi wake kama ilivyokuwa awali kwani jambo hilo kwanza linapelekea watu kuanza kufuatilia maisha yake ya mahusiano na si kazi zake za muziki.

Linah ni miongoni mwa wasanii wengi walioweka wazi penzi lao na watu kadhaa lakini mwisho wake hawakuweza kudumu kwa muda mrefu kwenye mahusiano hayo.

Hata hivyo kumekuwepo na tetesi kuwa ana uhusiano na rapper Bill Nass.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment