Baada ya miaka 46 ya ndoa, mwanamke mwenye miaka 72 amejifungua mtoto wa kwanza huko India na kuibua gumzo katika jamii inayomzunguka na kushangaza pia ulimwengu.
Daljinder Kaur amejifungua mtoto wa kiume baada ya kupata matibabu ya IVF kwenye kliniki za uzazi huko India.
Kaur amesema yeye na mume wake walikuwa karibu kukata tamaa ya kupata mtoto kutokana na umri wao na kuona kama Mungu amewalaani wasipate mtoto.
Amesema hatimaye Mungu amejibu maombi yao na wamepata mtoto na sasa wanajiona wamekamilika.
Amedai kuwa kuwa yeye na mume wake watamlea mtoto wao wenyewe kwasababu huyo mtoto amewapa nguvu mpya katika maisha.
Pia anawasihii wote wenye changamoto za uzazi wamuombe Mungu bila kuchoka…. na kusema “I can’t wait to be a grandma!!”.
Dkt Kanad Nayar, katibu mkuu wa chama cha upachikaji mimba nchini India anasema sheria ya kuamua umri wa juu ambao mwanamke anaweza kuruhusiwa kutumia teknolojia hiyo ni karibu miaka 55.
Daktari huyo anasema jambo la kuzingatiwa zaidi ni uwezo wa mwanamke kumlea mtoto hadi akomae.
“Ukimzaa mtoto lazima uweze kumlea mtoto kwa karibu miaka 20 hivi. Huwezi kujifungua mtoto kisha uwaache watu wengine wakimlea,” alisema Dkt Nayar.
Ni mara ya pili kwa mwanamke mkongwe kujifungua mtoto India. Awali, mwanamke wa miaka 70 alijaliwa mtoto nchini humo.
Lakini mwanamke huyo alifariki miaka miwili baadaye na sasa mtoto huyo anatuzwa na jamaa zake.
Blogger Comment