Hamisa Mobeto Akanusha Fashion Kuwa Uhuni

Hamisa Mobetto
Mwanamitindo Hamisa Mobeto amewataka wazazi kuuwaacha watoto wa kike na wa kiume waingie kwenye fashion na kuachana na dhana ya kwamba kufanya modeling ni uhuni.
Hamisa ameyasema hayo wakati akitoa maoni nini kifanyike ili kuboresha tasnia ya mitindo, na kutumia fursa hiyo kuwataka wazazi kuichukulia tasnia ya fashion kama moja ya sehemu ya ajira.
“Unajua Watanzania wengi bado hawajajua nini maana ya modeling , wengine wanadhani ni uchafu, uhuni, Tanzania kuna wanawake wazuri sana, kama wazazi wakiwaruhusu vijana wao kufanya modeling basi Tanzania tutafika mbali sana kwa sababu tuna warembo wengi sana,”
Sambamba na hilo mrembo huyo ameitaka serikali kuangalia tasnia ya fashion ambayo kwa sasa inatoa ajira kwa vijana wengi pamoja na kuitangaza nchi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment