Mourinho ambaye ni kocha wa zamani wa Chelsea, Inter Milan na Real Madrid alijiunga na United hivi karibuni huku akiahidi kuzoa kila kombe.
Kocha huyo mwenye miaka 53, amesema suala la kufuzu tu kwenye Ligi ya
Mabingwa Ulaya msimu ujao haliwezi kuwa na msaada kwake bali kutwaa makombe.
“Ninapozungumza kuhusu kutwaa makombe huwa sina masihara, naomba niseme tu kwamba nataka kutwaa makombe yote msimu huu.
“Nataka kila kitu, nataka kushinda kila mchezo kwa kucheza vizuri, kufunga mabao na sitaki kuona tunaruhusu kufungwa.
“Najua haya ni mambo magumu lakini sina shaka kwa kuwa nitayafanikisha kwa ustadi wa hali ya juu,” alisema Mourinho.
United wanakwenda China kwa ajili ya maandalizi yao ya msimu ujao ambao utaanza mapema mwezi ujao.
Blogger Comment