Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Hafsa Mossi auawa

amosozi
Hafsa Mossi.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi, Hafsa Mossi ameuawa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura leo.
Bi. Mossi, aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki katika serikali ya nchi hiyo, aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya Gihosha, eneo la Nyankoni.
Mbunge huyo aliwahi kufanya kazi na idhaa ya Kiswahili ya BBC.
mossi
Msemaji wa rais wa Burundi, Willy Nyamitwe amesema amesikitishwa sana na mauaji ya mwanasiasa huyo.
“Nimesikitishwa sana. Dadangu mkubwa Hafsa Mossi, mwanachama wa @EA_Bunge amefariki, amepigwa risasi na wahalifu. R.I.P #Burundi,”
Waziri wa Mambo ya Nje, Alain Aime Nyamitwe pia ameeleza kusikitishwa kwake na mauaji hayo.
“Nimehuzunishwa sana na mauaji ya leo #Bujumbura ya Mheshimiwa Hafsa Mossi, na mwanachama wa #EALA. Ni hasara kuu kwa taifa na #EAC,”..Chanzo BBC.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment