JB, Uwoya gumzo!

JB WOLPER (6)
Jacob Stephen ‘JB’ na Irene Uwoya wakijiachia.DAR ES SALAAM: Waigizaji wakubwa katika  filamu Bongo, Jacob Stephen ‘JB’ na Irene Uwoya, mwishoni mwa wiki walizua gumzo kwa baadhi ya watu waliohudhuria pati ya Black Tie ya mcheza sinema mwenzao, Wema Sepetu, iliyofanyika katika Ukumbi wa King Solomon, jijini Dar es Salaam.
JB WOLPER (4)Kilichosababisha gumzo hilo ni kitendo cha wawili hao kuwa karibu na mara kadhaa kushikana kama watu wenye uhusiano wa karibu, ambao ulionekana kuwashtua wadau wengi waliokuwa wamejazana ukumbini humo, ambamo Christian Bella alikuwa kivutio kikubwa katika burudani.
“Waone jamani, lakini wamependeza sana eeh. Lakini huyu JB si ana mke?
Namuonaga ni mtu wa kujiheshimu sana, sijawahi kusikia kuhusu maskendo, au na yeye wamo nini?” mmoja wa waliohudhuria onesho hilo ambaye hakufahamika jina lake alisikika akimsengenya.
JB WOLPER (5)Staa mmoja wa  filamu, ambaye baada ya kumgundua mwandishi wetu kuwa ni mmoja wa waliomsikia akiwazungumzia waigizaji hao, alimpiga mkwara na kutotaka jina lake liandikwe, alisema katika Bongo Muvi hakuna lisilowezekana, hasa watu wakiwa wamefurahi.
“Hapa lolote linaweza kutokea, kwani nani kamuambia kuna linaloshindikana chini ya jua? Kaka mkubwa anaweza kubadili matokeo wakati wowote, wakongwe hao,” alisema staa huyo.
JB WOLPER (7)Licha ya kuwa pamoja na kuonekana wenye furaha, pia waigizaji hao walikuwa ni miongoni mwa watu waliojitokeza na kutoa fedha nyingi kumtuza mwimbaji Christian Bella aliyetumia pia siku hiyo kuzindua CD yake ya miaka kumi katika muziki wa dansi nchini.
JB WOLPER (2)
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment