Mimba ya JOKATE yazua Kizaazaa

DAR ES SALAAM: Kizaazaa! Kufuatia mwanamitindo nyota Bongo na Miss Tanzania Namba 2, 2006, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kudaiwa kuwa na ujauzito wa Mbongo Fleva, Alikiba Saleh, mazito yameibuka kwa mademu waliowahi kusemekana ni ‘zilipendwa’ wa msanii huyo kusemwa kwamba, hawakuwa na uwezo wa kumzalia, Risasi Mchanganyiko linakuwa la kwanza kukudondoshea.
jokateChanzo makini kililiambia Risasi Mchanganyiko kuwa, warembo wanaodaiwa kuwa ni wapenzi wa zamani wa Kiba ni Gift Stanford ‘Gigy Money’, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ na Sabrina Omar ‘Sabby Angel’ kwamba hawakuwa na uwezo wa kuzaa, ndiyo maana hawakuweza kushika ujauzito wa staa huyo na kuishia kuachika tu.
MSIKIE HUYU HAPA
“Wapenzi wa zamani kina Gigy Money, Sabby Angel na Amber Lulu hawakuwa na uwezo wa kuzaa ndiyo maana hawakuwahi kuonekana wakiwa na ujauzito au kusikika kwamba walikuwa na mimba ikaharibika na sasa hivi hawataki hata kusikia habari za ujauzito wa Jokate hivyo tunamsifu Jokate kama ni kweli ana mimba ya Kiba.
kiba jokateJokate na mpenzi wake, Alikiba Saleh
“Mashabiki kibao wameonekana kufurahishwa na jambo hilo kwani wamemuona ni mwanamke mwenye ujasiri licha ya kwamba Kiba ana watoto wengine watatu kwa mama tofauti, lakini yeye (Jokate) hajaona tatizo kumzalia. Inaonesha ni jinsi gani anavyompenda Kiba, kwa hiyo ni mfano wa mwanamke wa kuigwa kutokana na ujasiri na msimamo wake,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata ubuyu huo kutoka kwa chanzo, Risasi Mchanganyiko liliwasaka wahusika hao waliotajwa kutoka kimapenzi na Kiba ambapo kila mmoja alitoa kauli yake huku wengine wakitoa kauli za kushambulia.
 GIGY MONEY ASEMA
Huyu ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumza na Risasi Mchanganyiko ambaye alisema maneno makali bila kuumauma midomo kwa Kiba na Jokate pia.
“Jokate azae tu hainihusu! Ninachotafuta mimi ni pesa, maana hao watoto wapo tu muda wowote nikitaka nitazaa maana kizazi ninacho. Wanaosema sina uwezo wa kuzaa hawajawahi kunipima, Kiba amebaki kuwa X (wa zamani) wangu tu na tumewahi kufanya mengi enzi hizo wanajuaje kama niliwahi kupata ujauzito ukaharibika?”
AHOFIA MANENO MAKALI KUHARIBU MIMBA YA JOKATE
“Sitaki kumpa maneno machafu maana kama Jokate ni mjamzito mimba ikatoka bure, yeye azae naona kawaida tu hainiumizi chochote. Kwanza baba mwenyewe Kiba mwenye watoto kibao nje, wala hainisumbui. Yeye Jokate ndiye amemuona Kiba wa maana awe baba mtoto wake, he! He!
“Azae naye tu, lakini ajue atakuwa mama wa watoto wengine watatu, wa kwake atakuwa wa nne. Mimi niponipo kwanza si kama Jokate alivyoamua.”
SABBY ATOA SABABU ZA KUMBANIA MIMBA KIBA
Kwa upande wake, Sabby alifunguka; “Wanaosema sina kizazi hawanifahamu vizuri, nina mtoto mkubwa tu ambaye nilipata kwa marehemu mume wangu ndani ya ndoa na anasoma darasa la kwanza. Kiba sikuzaa naye kwa sababu sitaki kuzaa nje ya ndoa, maana nitamnyima mwanangu haki ya msingi ya kulelewa na wazazi wote wawili, pia mimi ni mtoto wa Kiislam safi.
“Sijuti maana yalikuwa ni maamuzi yangu, sizai nje ya ndoa, sitaki kumkosea Mungu, Jokate kuwa mjamzito ni jambo zuri na la heri na Kiba ni baba mzuri sana kwa sababu ana watoto watatu na kila mmoja ana mama yake, na anawahudumia ipasavyo…teh! Teh!”
AMBER LULU ACHOMOA
“Mimi siwezi kulizungumzia hilo kwa sababu sijawahi kutoka na Kiba.”.
HII NI MIMBA YA PILI
Mwaka jana, Jokate aliwahi kuripotiwa kuwa na ujauzito wa mwanamuziki huyo, lakini ukachoropoka na kusababisha penzi lao kuyumba kwa muda lakini kwa sasa anadaiwa kuwa na ujauzito tena na mapenzi yao yanasemekana yapo motomoto!
JOKATE ATAFUTWA
Ili kuleta mzani wa habari hii, juzi, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Jokate kwa njia ya simu lakini ilikuwa bize wakati wote na alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS) hakujibu mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni.
SIKU CHACHE NYUMA
Siku chache nyuma, paparazi wa Global alimtumia meseji  Jokate kumuuliza kuhusu madai ya kunasa ujauzito ambapo alijibu: Siyo kweli. Lakini hao wanaosema nina mimba wananitakia mema maana ni jambo la heri.”
KIBA NAYE
Kiba naye alipotafutwa juzi kwa njia ya simu, hakupokea licha ya kupigwa mara kadhaa, utadhani alikuwa na Jokate ‘wakaambizana’ wasipokee!!
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment