Gari hilo lenye thamani ya shilingi milioni 200 lilikamatwa maeneo ya Mbezi-Africana jijini Dar likiwa na msala wa kuingizwa nchini kinyume na utaratibu sambamba na kutolipiwa kodi.
Jumatatu iliyopita, paparazi wetu aliyekuwa na taarifa za mnada huo, aliibuka kwenye yadi ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) iliyopo nyuma ya Jengo la Water Front jijini Dar ambapo ilipotimu saa tano na nusu asubuhi, mnada ulianza rasmi.
Kabla ya kuanza mnada huo matajiri zaidi ya hamsini walianza kuyakagua magari yaliyopo kwenye yadi hiyo ingawa mengi yaliyopigwa mnada yalikuwa katika yadi zingine ikiwemo ile ya Baridi, Mnazi Mmoja.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, mmoja wa wafanyakazi wa Yono Action Mart aliyevalia fulana na kizibao cha kampuni hiyo ambaye alikataa kutaja jina lake, alisema gari hilo zamu yake bado kwani walianza idadi fulani ya magari kutokana na wateja waliojitokeza.
Blogger Comment