HUYU HAPA:Jamaa Anayelipwa Pesa kwa kubikiri watoto na kufanya ngono na Wajane

MALAWI (1)Eric Aniva ‘Fisi ‘ mtajika aliyewabikiri zaidi ya watoto 10.
Malawi
KATIKA hali ya kawaida, tamaduni nyingi kote duniani mwanamke anapoolewa huwa ni fahari kubwa sana endapo akiwa ni bikira mathalan ni dhihirisho kwamba mwanamke huyo amelelewa na kutunzwa vyema na wazazi wake ama walezi wake, pia ni dhihirisho la usafi wa mwanamke.
Licha ya hayo yote, jamii moja nchini Malawi haithamini ubikira wa watoto wao wa kike, amini usiamini wazazi huwa wanamlipa mwanaume ambaye ni maarufu kama ”Fisi” kumbikiri binti yao punde tu anapopata hedhi yake ya kwanza kwa imani kuwa binti ambaye ni bikira ni mkosi kwa jamii!
MALAWI (2)Aniva huchemsha mizizi hiyo kabla ya kuanza kubikiri watoto kwa takriban siku 3 hivi.
Wazazi na jamii kwa jumla katika maeneo mengi ya kusini mwa Malawi wamekuwa wakishikilia tamaduni hii kwa miaka mingi sasa.


Kwa kawida ya mila zao, ”Fisi” ama wanaume wanaowabikiri watoto wakike huchaguliwa na wazazi kuwaondolea mikosi na huwa ni sherehe kubwa inayomtangulia binti kupelekwa unyagoni kisha kuwatembelea shangazi wake kabla ya kujulishwa kwa fisi.
Amini usiamini hao mafisi hulipwa takriban dola $7 (sawana pesa za Kitanzania shilingi 15,000/=) kwa kila kitendo cha ngono na hao mabinti ambao wengi huwa na kati ya umri wa miaka 11-14.
MALAWI (1)Fisi mmoja maarufu katika kijiji cha Nsanje, Eric Aniva ameiambia BBC kuwa hajui idadi kamili ya wasichana ambao amewabikiri.
”Kwa kweli mimi nimewabikiri zaidi ya wasichana 104”
”Hiyo ndio tamaduni zetu”


”Hapa mwanamke akifiwa lazima aje kwangu nimuondolee mkosi hata kabla ya kuzikwa kwa mumewe”.
”Mwanamke akiavya mimba pia kabla hajarejelea maisha yake ya kawaida ama hata kushiriki ngono na mwanamume mwengine lazima aje kwangu nimsafishe”. alisema Fisi huyo.
MALAWI (3)Aniva na familia yake
Aniva ambaye ana umri wa takriban miaka 40 ana wanawake wawili na watoto 5, anasema kuwa pale anaposhiriki ngono na watoto hao huwa anapewa muda wa siku 3 hivi kumsafisha na kumuondolea mkosi. Kulingana na tamaduni zao, ikiwa mwanamke ama binti anakataa asibikiriwe huwa wanaamini kuwa jamaa zao watafuatwa na mikosi na magonjwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment