VIDEO Queen ambaye anabamba kwa sasa akiwa pia ni mwigizaji wa tamthilia ya Kelele, Gift Alphonce ‘Gigy Money’, anadaiwa kuuza mwili wake kutokana na kauli zake kwamba yuko kipesa zaidi.
Akizungumza na BINGWA jana, mrembo huyo mwenye mvuto wa aina yake, alithibitisha hilo akisema kuwa hajali watu wanaosema, anachoangalia ni dau kwa kuwa yeye si Mtume wa Mungu na anachokitaka ni fedha tu.
“Dau lako tu, ukija na dau la kuridhisha, basi umening’oa, niko kikazi zaidi na ninatafuta hela, hivyo wanaosema waache waseme, yangu mimi yananiendea na bora mimi kuliko wanaojifanya watakatifu,” alisisitiza.
Mrembo huyo ambaye kwa sasa amelikamata Jiji la Dar es Salaam kutokana na vituko vyake vya kila kukicha, amekuwa akisemwa baadhi ya wanamitindo wenzake kuwa hayuko kikazi bali yuko kichangudoa na hana muda mrefu atapotea katika ‘game’.
Blogger Comment