Mama akamatwa na mirungi 'Airport"

MIRUNGI- PICHA NA GLOBAL PUBLISHERS (2)Aziza Suleiman Ally
Jeshi la Polisi Viwanja vya Ndege Tanzania wakishirikiana na maafisa usalama wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  (JNIA), wamemtia mbaroni mama mmoja aliyetambulika kwa jina la Aziza Suleiman Ally (pichani), mkazi wa Mombasa Kwamchina,  Zanzibar akiwa na mirungi.
Imeelezwa kuwa Aziza alinaswa uwanjani hapo Julai 13, mwa huu saa nane mchana akiwa ameficha mirungi hiyo sehemu mbalimbali ya mwili wake kama vile kwapani, kwenye matiti na sehemu za siri.
MIRUNGI- PICHA NA GLOBAL PUBLISHERS (1)Mirungi
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Viwanja vya Ndege Tanzania, ACP Maltin Otieno alisema ni kweli tukio hilo lilitokea.
Kamanda Otieno alisema kuwa Aziza alinaswa uwanjani hapo akiwa anajiandaa kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Msumbiji kwenda nchini humo akiwa ameficha mirungi mibichi pakiti nne sehemu mbalimbali za mwili wake.
MNIGERIA-ANASWA-NA-UNGA-3Kamanda wa Viwanja vya Ndege Tanzania, ACP Maltin Otieno
“Ni kweli sisi jeshi la polisi kwa kushirikiana na Usalama wa Taifa wa uwanjani hapa, tumemkamata Aziza Suleiman Ally (34) mkazi wa Mombasa Kwamchina Zanzibar raia wa hapa Tanzania akiwa na mirungi pakiti nne za uzito wa kilo nne akiwa amezificha sehemu mbalimbali za mwili,” alisema kamanda huyo.
Hata hivyo, alisema kuwa thamani ya mirungi hiyo bado haijajulikana na kutoa honyo kali kwa wale ambao wanajidanganya kutaka kupitisha madawa ya kulevya uwanjani hapo kwani ni lazima watakamatwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment