Kwa mujibu wa majirani, mtoto huyo ambaye hata mahudhurio yake shuleni si mazuri, amekuwa katika mateso hayo ya kupigwa mpaka kujeruhiwa kwa muda mrefu lakini majirani walikuwa wakishindwa jinsi ya kumnasua kuzingatia kuwa, anayedaiwa kufanya vitendo hivyo ni mama yake.
“Kila siku anampiga huyu mtoto. Unayaona hayo majeraha? Yote yametokana na kipigo ambacho anakipata kutoka kwa mama yake,” alisema mama Donata huku akimgeuzageuza mtoto huyo sehemu ya shingo ili kuonesha majeraha hayo.
“Nilikuwa nafanyiwa unyama wa kutisha na mama, ananipiga, ananifinya, ananigongesha ukutani mpaka natokwa na damu nyingi hadi zinakauka zenyewe.
“Siku nyingine aliniambia ataniua halafu aniweke kwenye kiroba na kwenda kunitupa porini. Chakula sili nikashiba, mengine hayaelezeki,” alisema mtoto huyo.
Juzi, Uwazi lilimtafuta mama wa mtoto huyo kwa njia ya simu lakini ikapokelewa na mwanaume aliyesema ni mume au baba wa mtoto huyo ambaye alisema:
“Mimi siwezi kusema lolote kuhusu ishu hiyo kwa sababu suala lenyewe lipo polisi.”
Uwazi: “Basi uje ofisini kwetu tuliongelee hili suala la mtoto wako.”
Baba: “Mimi huko ofisini kwenu siwezi kuja.” (akakata simu).
Hata hivyo, kwa mujibu wa mjumbe wa nyumba kumi, suala hilo limepelekwa Kituo cha Polisi Kimara na kuandikishwa kwa faili lenye kumbukumbu KIM/2858/016 TAARIFA. Pia, akina mama hao walimpeleka mtoto huyo kwenye Zahanati ya Serikali, Kimara na kupewa fomu ya polisi namba tatu (PF3) yenye namba KMR/10791/2016 SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI.
Blogger Comment