SORRY MADAM -Sehemu ya 5 & 6 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
“Nipe namba ya mumeo”
“Eehee”  
“Nipe namba ya mumeo, hujanisikia?”
Phidaya kwa uwoga akaichukua simi yake aliyo kua ameiweka pembeni ya glasi iliyo jaa juisi ya embe, vyote kwa pamoja vikiwa juu ya meza ya kioo iliyopo ndani ya kibanda hicho. Kwa kutetemeka Phidaya akaitafuta namba ya simu ya mumewe na kumuonyesha Mzee Godwin, ambaye taratibu akainadika kwenye simu yake na kuipiga namba hiyo.                                                                     

ENDELEA
“Mwanangu Phidaya”
Mzee Godwin alijibu kwa kujiamni, jambo lililo zidi kumchanganya Eddy ambaye mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbio, kwani uhasama wake na Mzee Godwin ni mkubwa kupita kiasi.
“Nakuomba usifanye chochote kwa mke wangu, nakuomba baba yangu”
“Mmmm leo ndio unajua kwamba mimi ni baba yako?”

Mzee Godwin aliendelea kuzungumza kwa dharau jambo lililo zidi kumpagawisha Eddy, kwani umbali kutoka Dododma hadi Dar es Salaam, unachukua muda mwingi sana kuweza kufika mbaya zaidi bado anakipengele cha kumalizia bungeni kuweza kujibu maswali atakayo ulizwa kama waziri wa ulinzi, ambaye amechukua majukumu ya kusimamia sekta zote za jeshi kuanzia polisi hadi jeshhi la kujenga taifa, na wizara ya mambo ya ndani ikatolewa katika usimamizi wa jeshi la polisi na kubaki ikiendelea kusimamia mabo mengi na si jeshi la polisi, ambalo lilihamishiwa kwenye wizara ya ulinzi moja kwa moja

“Leo, mke wangu atanipikia chakula kizuriii, kwahiyo usiwe na wasiwasi wowote, wewe endelea kupiga kazi”
Baada ya kuzungumza hivyo mzee Godwin akakata simu, na kuizima kabiasa kisha akamtazama Phidaya ambaye bado anaendelea kutetemeka mwili wake wote kwa woga mwingi ulio mtawala. Madam Mery akatoa kitambaa cheupe kilicho kunywa vizuri ambacho walikipulizia madawa ya kulevya kisha akamkabidhi mzee Godwin.

Mzee Godwin akamsogelea Phidaya sehemu alipo na kumziba na kitambaa hicho puani mwake, Phidaya akajitahidi kushindana nguvu na mkono wa mzee Godwin ulio mziba puani ila akajikuta akishindwa, huku nguvu zikianza kumuishia taratibu taratibu hadi akalala fofofo.

Mzee Godwin akambeba Phidaya begani na kuingia naye ndani, ambapo wakamlaza kwenye moja ya sofa kubwa walilo likuta hapo sebleni, kisha akaanza kuingia chumba kimoja baada ya kingine kuweza kutafuta funguo ya gari walizo  zikuta zimewekwa sehemu maalu za maegesho. Madam Mery yeye akawa na kazi ya kuchungulia madirishani ili kuweza kuona nje kama kuna mtu anaingia aweze kumstua mzee Godwin ambaye anaendelea kuwajibika na utafutaji wa funguo hizo.

Mngurumo wa gari, ukisimama nje, ukamstua Madama Mery aliye kuwa ameketi kwenye sofa, kila mara akitazama tazama saa yake ya mkononi, akihesabu muda jinsi unavyo kwenda. Akasimama kwa haraka na kwenda kuchungulia dirishani, akamuona mtoto mdogo wa kiume akishuka kwenye gari hilo aina ya BMW Z8, huku akiwa ameongozana na mtu anaye onekana kama ni dereva.

Kwa jinsi mototo huyo anavyo fanana na Eddy moja kwa moja Madam Mery akagundua kwamba huyo ni mtoto wa Eddy. Kwa haraka Madam Mery akapandisha ngazi za kuelekea gorofani, ambapo ndipo alipo Mzee Godwin. Kwa bahati nzuri akakutana na Mzee Godwin akitoka kwenye moja ya chumba akitaka kuelekea kwenye chumba kingine.

“Vipi?”
“Kuna watu wanakuja”
Madam Mery alizungumza huku akihema kwani, alizipandisha ngazi hizo zipatzo thelathini kwa kukimbia
“Kina nani?”
Mzee Godwin alizungumza huku akitembea kuelekea sehemu ambapo ataweza kuiona seble vizuri. Mzee Godwin akamshuhudia mjukuu wake Junio  akiingia huku nyuma akiwa ameongozana na dereva wa gari aliye mleta. Junio akamkimbilia mama yake aliye lala kwenye sofa na kumrukia kwa lengo la kumstua, ila hakufanikiwa kumstua mama yeka kwani hakuweza kustuka wala kutikisika, jambo lililo mpa wasiwasi mwingi Junio na kumfanya anze kulengwa lengwa namachozi.

  ***
    Eddy akajaribu kuipiga tena namba ya Mzee Godwin iliyo toka kumpigia muda mchache ulio pita ila haikupatiokana, wasiwasi mwingi ukazidi kumsumbua Eddy, akajaribu kupiga kwa mara ya pili ila hali ikawa ni ile ile ya kuto kupatikana kwa namba hiyo. Akajaribu kuipiga namba ya mke wake, ikaita pasipo kupokelewa.
“Mungu wangu?”
Eddy alizungumza huku akizunguka zunguka ndani ya chumba huku jasho jingi likimwagika mwilini mwake, na kujikuta akifungua vifungo vyote vya shati lake. Eddy akafungua mlango na kuanza kutembea kwenye kordo ndefu, ya hoteli aliyo fikizia akielekea sehemu  ya mapokezi, kabla hajafika akakutana na askari wake anaye mlinda
“Vipi muheshimiwa”
“Nahitaji kwenda, Dar sasa hivi”
Eddy alizungumza kwa haraka huku akizidi kupiga hatua kuelekea nje ya hotel hiyo kwenda kwenye maegesho ya magari.

“Unakwenda kufanya nini muheshimiwa?”
“Mke wangu ametekwa, fanya hivi mpigie simu naibu waziri, mkabidhi mafaili yangu yote na kipindi cha pili yeye ndio atajibu maswali sawa”
“Sawa mkuu”
Eddy akafika kwenye gari lake, na kumkuta dereva akiwa amejilaza.
“Shuka nipishe niendeshe”
Eddy alizungumza na kumfanya dereva wake kustuka kutoka usingizini
“Mmmmm”
“Hujanisikia au, nimekuambia kwamba zunguka upende wapili wa gari, tunahitaji kwenda Dar es Salaam sasa hivi”
“Muheshimiwa ni jukumu langu mimi kukuendesha”
“Wewe mzee, mimi ni nani yako? Nimekuambia nipishe”
Eddy alizungumza kwa hasira na kumfanya mzee Selemani Mbogo, kutii amri ya bosi wake, akashuka kwa haraka na kuzunguka upende wapili wa gari, askari akataka kuingia kwenye gari ila Eddy akamzuia
“Wewe baki, hakikisha document zangu zote unampa naibu waziri sawa?”
“Sawa mkuu”
“Naomba bastola yako”

Hapo askari akasita kidogo kuichomoa bastola yake aliyo ichomeka kiunoni mwake, kwa ishara Waziri Eddy akamuomba amkabidhi bastola hiyo, taratibu askari huyo akaichomoa na kumpa bosi wake. Eddy akaipokea na kuifunga mlango wa gari, akaliwasha, akakanyaga mafuta pamoja na breki na kuzifanya tairi za gari hilo kuserereka, na kutoa moshi mwingi, kisha akaachia breki na kulifanya gari hilo kuchoka kwa kasi, na kuwafanya watu wlaiopo katika eneo la hoteli kushangaa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment