MWANAFUNZI
Marco Limbe(14) aliyemaliza darasa la saba mwaka huu katika shule ya
msingi Yitwimila iliyoko kata ya kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu
amelazwa katika kituo cha afya Busega mara baada ya kuchalangwa mapanga
kichwani na mdomoni na mwalimu wake.
Tukio
hilo limetokea jana majira ya saa 11.30 jioni wakati mwanafunzi huyo
alipokuwa akirejea nyumbani kwao akitokea katika malisho ya mifugo ndipo
alipokaribia katika shamba la mwalimu Pendo Gabriel ndipo mwalimu huyo
alimkamata kijana huyo na kuanza kumchalanga kwa panga na kupelekea
kijana limbe kupoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 mara baada ya
kufikishwa katika kituo cha afya Busega.
“Shuhuda
wa tulio hilo aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Manoga anaeleza
kuwa ilikuwa kama mchezo lakini kumbe ni kweli kwani niliona mifugo ya
limbe iliyokuwa ikielekea nyumbani na huku limbe akiwa nyuma ya mifugo
hiyo katika barabara ambalo liko karibu na maeneo ya shule ghafla
nilimuona mwalimu pendo wakishikana na kijana huyo na ndipo nikamuona
akiwa na panga na kuanza kumchalanga”
Nilikimbia
katika tukio na kutoa msaada kwa wote lakini mara watu walijaa na
kuanza kumshambua mwalimu Pendo kwa kumpiga ingawa jaribio hilo
lilikwama mara baada ya mwenyekiti wa kijiji hicho mshemas bahai.
Mwandishi
alikwenda katika kituo cha afya cha Nyashimo na kujionea hali mbaya kwa
kijana Limbe ambaye alikuwa amepoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 bila
kujitambua na huku akiwa anaongezewa drip na kwa pembeni mwalimu Gabriel
naye akipata matibabu ya jeraha lake kichwani amabolo alishambuliwa na
wananchi na huku akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la piolisi.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio mwenyekiti wa Sogesca Bahai Mshemas alisema kuwa
sikukuu ya kuzaliwa kwa yesu imekuwa ni mbaya katika kijiji chake mara
baada ya wananchi walio na hasira kali kufanya shambulio la kumshambulia
mwalimu Pendo kwa kosa la kumchalanga na panga mwanafunzi wake
aliyekuwa akitokea kwenye malisho na kupita karibu na shamba lake la
mahindi.
Aliongeza
kuwa alifanikiwa kuwatuliza wananchi wa kijiji chake na kuanza kufanya
mikakati ya kuwapeleka kituo cha afya ili wapate huduma za matibabu.
Aidha Mshemasi aliongeza kuwa walifika polisi na kuandikiwa barua ya kwenda kutibiwa wote wawili mwalimu pamoja na mwanafunzi.
Kwa
upande wake kaimu mganga mfawidhi wa kituo hicho cha afya Dk Ayubu
Ismail alithibitisha kuwapokea kwa majeruhi hao na kudai kuwa kijana
limbe ndiye aliyekuwa na hali mbaya zaidi kuliko mwalimu pendo.
Aliongeza
kuwa kijana ameshonwa nyuzi 9 katika sehemu zake zote alizopatwa na
majeraha na huku mwalimu yeye akiwa ameshonwa nyuzi 6.
“Ni
kweli Limbe alikuwa ametokwa na damu nyingi sana na hivyo kumpelekea
kupoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 lakini hali yake inaendelea vizuri
alisema Dk Ismail”
Chanzo: Rweyunga
Blogger Comment