VIDEO:Shilole ‘Awaka’ Kisa Penzi na Jay Moe

MREMBO ambaye jina lake liko juu kwa sasa kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ hivi karibuni amewaka baada ya kubanwa maswali juu ya tetesi za uhusiano wake na Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’.

Akistorisha na Uwazi Showbiz, Shilole alifunguka kuwa hana uhusiano na mkali huyo wa ngoma ya Pesa Madafu na hajawahi kufikiria kutoka naye na anawashangaa watu wanaomhusisha kuwa kwenye mahaba na Jay Moe.

“Watu bwana wanashindwa kufuata yao wanakalia kuchonga yawenzao, mimi Jay Moe ni kaka yangu, tumeshibana na hatuna uhusiano wowote,” alisema Shilole.

Kwa upande wa Jay Moe amefunguka kupitia kwenye mitandao ya kijamii juu ya kuzisikia tetesi za yeye kutoka kimapenzi na Shilole, amedai pia hazina ukweli wowote maana mwanadada huyo ni mshikaji wake wa karibu tu!

TAZAMA VIDEO HAPA:
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment