Ufuatilia umeonyesha kuwa msanii huyo amekuwa akimposti Mwarabu huyo na kwamba kuna kila dalili ni mtu wake aliyerithi mikoba ya aliyekuwa mumewe, Gardner Habash.
“Nyie kama vipi fuatilieni kwa makini kwenye Instagram yake, mtagundua tu ukweli, kuna kitu maana hata akimposti huyo jamaa huwa anaweka maneno yenye utata, hataki kufunguka moja kwa moja kama ni mpenzi wake au vipi,” kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa mrembo huyo kupitia simu yake ya mkononi, iliita bila kupokelewa lakini mmoja wa mameneja wake alisema mwanaume huyo ni rafiki wa karibu wa Jide na kama kutakuwa na lolote, atafafanua baadaye.
“Ni rafiki yake tu na nisingependa kumtaja jina lake maana sidhani kama ni jambo zuri, nyie msiwe na wasiwasi, kila kitu kitakuwa wazi tu muda muafaka utakapowadia, najua watu wengi mnataka kumjua shemeji mpya, wawe wavumilivu tu watamjua,” alisema meneja huyo huku akiomba hifadhi ya jina.
Blogger Comment