USHUHUDA WA THEOFLIDA WA YESU : NILIMLISHA MUME WA MTU, LIMBWATA LA NYAMA YA BUNDI.
Nawasalimu wa jina la YESU, jina kuu kupita majina yote. Jina langu ninaitwa Theoflida , ni mwanamke mwenye umri wa miaka 38 mkaazi wa Mbezi ya Kimara jijini Dar Es Salaam, japo kiasili ni mwenyeji wa wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro..
Nime amua kuandika waraka huu kwa madhumuni makuu mawili, kwanza ni kushuhudia MATENDO MAKUU ambayo YESU AMENITENDEA na pili, ni kuwa hasa wanawake wenzangu kutojihusisha kabisa na masuala ya WAGANGA WA KIENYEJI kwa sababu waganga wa kienyeji ni MAWAKALA WA KAZI ZA SHETANI HAPA DUNIANI na ni MASHETANI KABISA!...
Nitaanza kwa kuelezea kisa kilicho nipelekea kuingia kichwa kichwa kwenye mikono ya wakala wa shetani..
Nilikuwa nimepanga chumba kimoja maeneo ya Tabata Mawenzi huku nikijihusisha na biashara ya genge. Jirani na nyumba niliyokuwa nimepanga, aliishi mwanaume mmoja na mke wake. Mwanaume huyu jina lake linaanzia na herufi K hivyo katika maelezo yangu nitakuwa nikimtaja kwa herufi K.
K alikuwa ni mwanaume mwenye mafanikio makubwa katika maisha mwenye kazi nzuri. Alikuwa na nyumba zaidi ya moja, magari ya kifahari. viwanja , mashamba, na miradi mbalimbali iliyokuwa ikimlipa vizuri sana. Kwa ufupi K alikuwa tajiri mwenye maisha mazuri.
K na mke wake wote walikuwa wenyeji wa wilaya ya Muleba,mkoani Kagera . Ndoa ya K na mkewe ilikuwa na umri wa mwaka mmoja...
K na mke wake waliishi maisha mazuri sana....Kwa sababu ya ugumu wa maisha yangu, nikajikuta naanza kutamani maisha ya mke wa K.. Nikawa natamani mimi ndo ningekuwa mke wa K na kufurahia maisha vile mke wa K alivyo kuwa akifurahia. Nilimuona mke wa K kama mtu mwenye bahati sana na kutamani bahati hiyo iwe yangu.
Baada ya wazo hili kukomaa ndani ya nafsi yangu, nikaanza kutafuta njia ya kumteka K kimapenzi na kuchukua nafasi ya mke wake. Njia pekee niliyo ona inafaa, ni kutumia uchawi.
Sasa basi, kuna rafiki yangu mmoja, anaitwa Pamela. Pamela alikuwa anapenda sana mambo ya waganga waganga, kwa hivyo alikuwa anawajua waganga wengi. Hata katika biashara yangu ya genge, alishanipeleka kwa waganga kadhaa kwa ajili ya kupata dawa ya mvuto wa bishara yangu..
Nilipo mfuata Pamela, akaniambia kuna mganga mmoja, ni mkali sana wa mambo ya mapenzi.. Mi mwenyewe nina mpango wa kumtafuta lakini najipanga kwanza kwa sababu bei zake ni kubwa.
Pamela akasema alimfahamu mganga huyo alipokuwa katika kijiji cha Mwalusembe, wilayani Mkuranga.. Siku hiyo kuna fumanizi lilitokea, mwanaume alikuwa anatembea na mke wa mtu, kumbe huyo mwanamke alikuwa amewekewa tego, huyo mwanaume alipo muingilia mwanamke huyo, wakawa wamenasana.. Baadae ikatafutwa namba ya simu ya mume wa mwanamke. Mume alipofika kufumania, akakuta mke wake amenasana na mgoni wake.. Akaitwa huyo Mganga kwa sababu ndie aliye weka hilo tego, alipofika eneo la tukio alifanya uganga wake, wale wagoni wakawa wameachana.. Tukio hilo lilivuta watu wengi sana.. Kwa hiyo Pamela anasema, alimjulia mganga huyu kwenye tukio hilo... Akafanikiwa kutafuta na kupata namba zake.
Pamela akanipa namba za simu za mganga huyo, nilivyo mpiugia akasema yupo Handeni kikazi ila baada ya siku tatu atakuwa Bagamoyo ambapo atakaa hapo kwa mwezi mzima aki agua watu wenye matatizo mbalimbali.
Kweli baada ya siku ya tatu, nikaenda hadi Bagamoyo kuonana na huyo mganga ambaye jina lake tu ni kufuru kubwa kwa Mungu.,. Yeye anajiita MUNGU WA KABILI ambayo tafsiri yake ni MUNGU WA PILI. Lakini pia nilishangaa kumuona mganga mwenyewe anaokena bado kijana ambaye sidhani kama ana fikisha miaka arobaini

Blogger Comment