TAREHE KAMA YA LEO JULAI 11 2015 USIKU

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari usiku huu nje ya ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma, mara baada ya kumalizika kwa Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichokaa kupitisha majina matano ya wagombea Urais yatakayopelekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM kujadiliwa hapo saa nne asubuhi.








Nape hakutaja majina hayo ya wagombea waliopita kwenye tano bora na kusema atataja asubuhi.
Muda mfupi baada ya Katibu wa NEC itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari, walitoka wajumbe watatu wa Kamati Kuu ambao ni Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mh. Sophia Simba na Mh. Adam Kimbisa ambao walizungumza na waandishi wa habari juu ya walichokizungumza kwenye kikao hicho, ambapo wao walisema wamegomea makubaliano ya majina yaliyopitishwa kwenye kikao hicho kwa madai kwamba Kikao kimekiuka taratibu za uchujaji wa majina hayo. kwani yalijadiliwa majina machache tu na kupitishwa kwenda tano bora, lakini nao hawakuyataja majina hayo.




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment