DAR ES SALAAM: Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani cha Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ ameweka wazi kuwa mwanaume aliyenaye siyo mume wa mtu bali ni halali yake tofauti na watu wanavyodai kuwa amepora mume wa mtu.
Akizungumza na Wikienda, Dida alifunguka kuwa anawashangaa wanaochonga kuwa anamiliki mume wa mtu, jambo linalomfanya awaone watu hao kuwa wanazungumza vitu bila kujua undani wake.
“Hakuna cha mume wa mtu hapa. Mwanaume niliye naye ni wangu peke yangu, angekuwa wa mtu angekuwa kwa mwenyewe lakini hivi sasa niko naye kila kona,” alitamba Dida.
Dida ambaye alishaolewa mara tatu na kuachika alisema kuwa ndoa siku zote ni bahati ya mtu hivyo anafurahia Mwenyezi Mungu kumjalia kuwa na mwanaume huyo.
Blogger Comment