Chadema watangaza mikutano ya hadhara Na Maandamano Nchi Nzima kuanzia Septemba Mosi....

Kufuatia kile walichokiita 'matukio ya ukandamizaji wa haki na demokrasia',   Chadema kimetangaza Septemba Mosi mwaka huu kuwa siku ya mikutano ya hadhara nchi nzima.

Chama hicho pia kimezindua Operesheni Ukuta (Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania),  huku kikiwataka wananchi wote waliokumbana na 'rungu'  la Serikali ya Awamu ya Tano kuungana na Operesheni hiyo,  wakiwemo mama ntilie na waendesha bodaboda.

Chama hicho kimetaja mambo 11 kinachodai kuwa yamefanywa na Serikali bila kufuata sheria na kanuni za nchi,  likiwemo la kuzuiwa kwa shughuli za kisiasa na kutaja sababu 24 za kuibuka na Operesheni Ukuta
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment