Auawa Kwa Kukatwa Kichwa..Kiwiliwili Chatelekezwa Bila Kichwa

Mtu mmoja amefariki dunia kwa kukatwa kichwa na kiwiliwili chake kutelekezwa kichakani katika Kijiji cha Rushwa, Kata ya Mushabago, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Buyango, Gasper Joseph amesema wamelazimika kuita wananchi ili kuutambua mwili wa marehemu.

Amesema licha ya kiwiliwili kutelekezwa kwenye eneo la kichaka, kichwa cha marehemu huyo wa kiume hakikuwapo kwenye eneo hilo jambo ambalo alilosema limeleta hofu kwa wananchi.

“Nimeita watu na walikusanyika, hata hivyo walishindwa kuubaini mwili huo kwa kuwa kichwa chake hakikuonekana. Mwenyekiti wa Kijiji cha Rushwa alitoa taarifa polisi kwa ajili ya hatua zaidi ili turuhusiwe kuzika,” amesema Joseph.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment