Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka aliwataja waliokufa katika ajali hizo kuwa ni Ahmed Musa (65) mkazi wa Kintinku, Manyoni, Saidi Arafat (30) mkazi wa Dodoma, Charles Mesomapya (52), Juma Mboje (43) na Adam Sadik (36) wote wakazi wa Muhalala, Manyoni.
Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Adam Seif (63) na Abdallah Mohamed (62) wote wakazi wa Manyoni mjini.
Ajali zote mbili zilitokea juzi katika maeneo tofauti wilayani humo. Katika ajali ya kwanza iliyotokea saa 3.45 eneo la Tambukareli mjini Manyoni kwenye barabara kuu ya Manyoni – Dodoma, dereva Geofrey Msengeni akiwa na gari la mafuta T 373 BAP/ T 703 AFR aligongangana na Toyota Noah T 159 AZX na kusababisha vifo vya watu wawili.
Alisema katika ajali ya pili iliyotokea saa 1.00 usiku kwenye mlima mdogo wa Muhalala, dereva Leo Kariwa akiendesha basi T 163 BUS mali ya Osaka aliwakanyaga hadi kufa waenda kwa miguu watatu waliokuwa wakitoa msaada kwa gari nyingine iliyoshindwa kupanda mlima huo.
Chanzo cha ajali zote mbili ni uzembe wa madereva wa lori na gari hilo la abiria kuacha kuzingatia matumizi mazuri ya barabara.
Blogger Comment