ILIPOISHIA
“Unanidai shilling ngap?”
Mzee Godwin alizungumza huku akitoa pochi yake mfukoni, huku macho yake yote yakiwa kwa mama Eddy.
“Elfu hamsini”
Akachomoa
noti tano za elfu kumi kumi, nakumkabidhi dereva bodaboda pasipo
kumtazama, kisha akaanza kupiga hatua kuelekea alipo Mama Eddy, huku
taratibu hasira kali dhidi ya mke wake huyu ikiongezeka na kujikuta
akiichomoa bastola yake tayari kwa kumpiga risasi.
ENDELEA
Mama Eddy baada ya kuzungumza na simu, akaingia ndani ya hospitali na
kumfanya Mzee Godwin kusimama kwenye moja ta gari lililo egeshwa kwenye
maeneo haya huku macho yake akimsindikiza mke wake huyo, ambaye
alimshuhudia akizungumza na Eddy kisha wakaondoka
“Eddy Eddy Eddy”
Mzee
Godwin alizungumza huku akiwa amekasirika, tukio kubwa linalo muuliza
kichani mwake ni pale anapovuta picha jinsi pacha mwenzake alivyo kuwa
akifanya mapenzi na mke wake huyo, jambo linalomfanya kuzidi kumchukia
Eddy
“Nitakuua kwa mkono wangu mimi mwenyewe”
Mzee
Godwin alizungumza huku akiwashuhudia Eddy na mama yake wakitoka tena
nje ya hospitali huku wakiwa na Junio, aliye bebwa mikononi mwa Eddy
akionekana kupitiwa na usingizi. Gari la mama Eddy likafika sehemu
walipo simama huku kukiwa na dereva ndani yake.
“Nitakuja basi asubuhi, kumuona mgonjwa. Ngoja nikamlaze huyu chekbud wako”
“Sawa mama, usisahau kuja na chakula”
“Sawa nitakiandaa mimi mwenyewe”
Mama Eddy akaingia siti ya nyuma alipo lazwa Junio aliye jichokea kwa usingizi.
“Mama kumbuka hajala huyo akifika ale”
Eddy
alizungumza huku gari la mama yake likiondoka taratibu, Eddy
akalisindikiza kwa macho gari hilo hadi linatoka kwenye geti, Macho ya
Eddy yakashuhudia mtu akiwa amejibanza kwenye moja ya gari huku
akionekana kama anachunguza kitu fulani, kutokana na mwanga hafifu ya
eneo la maegesho hakuweza kumuona sura yake.
Eddy
akataka kwenda ndani ila roho yake ikasita kabisa na kujikuta akianza
kupiga hatua za taratibu kwenda sehemu lilipo gari hilo. Mzee Godwin
akatabasamu, alipo kua anamuona Eddy akija katika eneo alipo jificha
yeye. Akaishika bastola yake huku akimsubiria kwa hamu kubwa, Eddy afike
ili amuulie mbali
Gafla
simu ya Eddy ikaita na kumfanya asimame na kuitoa mfukoni mwake, na
kukuta ni namba ya spika wa bunge, akaitazama kwa sekunde kadhaa, kisha
akaipokea
“Ndio kiongozi habari”
Eddy akuzungumza huku akitazama pembeni upande ambapo hayupo mtu aliye hitaji kumuona ni nani na kwanini anajificha
“Salama vipi, mbona umekimbia bila taarifa?”
“Kuna matatizo yakifamilia ilinibidi niwahi kuyatatua”
“Kwema lakini?”
“Hapana
si kwema kiongozi, kwani mke wangu alivamiwa na majambazi na kumuwekea
sumu, pia nikakuta mwili mwengine wa rafiki wa karibu ukiwa ndani ya
nyumba yangu, naye akiwa amepigwa risasi”
“Aisee, basi mimi nilijua kwamba umekimbia maswali”
“Hapana kiongozi”
“Pole sana, vipi polisi umewataarifu?”
“Bado, ila hili swala nitalimaliza kimya kimya”
“Basi kama ni hivyo, ila nikusifie kwa vidonge vyako vya leo, Umeniburudisha japo nilikuwa ninajikaza”
“Ni moja ya kazi yangu”
“Basi endelea na majukumu ukiwa saswa utaniambia”
“Sawa kiongozi”
Eddy
akakata simu na kuzunguka sehemu alipo hisi kuna mtu, ila hakukuta mtu
yoyote aliyepo kwenye eneo hilo. Kumbe kitendo cha Eddy kuzungumza na
simu, ikawa ni nafasi kubwa sana kwa Mzee Godwin kutembea kwa hatua za
haraka na kuingia kwenye jembo moja la kuhifadhia nguo, ikiwemo mashuka,
neti, na mavazi ya kidaktari
“Kumbe huyu mwanamke hajafaa, nilazima nimuue”
Mzee
Godwin alizungumza baada ya kumsikia Eddy akidai kwamba Madam Mery
hajafa. Mzee Godwin akavaa moja ya koti la kidaktari akachukua na kipimo
cha kupimia mapigo ya moyo, kisha kwa haraka akaanza kupita wodi moja
baada ya nyingine ya wagonjwa mahututi
Halikuwa ni jambo la kustukiwa mara moja kwamba yeye sio dokta, hii
nikutokana na wingi wa wafanya kazi katika hospitali hii, huku wengine
wakiwa wameingia zamu ya usiku wakiwapokeza wezao walio fanya kazi kutwa
nzima. Eddy akapiga namba za Mzee Seleman aliye kuwa akisimamia
ufanyiwaji wa oparesheni wa Madam Mery kutolewa risasi
“Ndio bosi”
“Hali ya mgonjwa inaendeleaje?”
Eddy alizungumza huku akiingia ndani, kuelekea kwenye chumba alicho lazwa mke wake
“Bado madaktari wanaendelea kuzitoa risasi, nipo kwa nje hapa ninachungulia kwenye kioo cha mlangi
“Sawa hakikisha haumruhusu mtu kuwa karibu ya mgonjwa zaidi ya madaktari, au nikuongezee nguvu ya ziada?”
“Hapana”
“Sawa fanya hivyo”
Eddy
baada ya kumaliza kuzungumza na mzee Selemani Mbogo, simu yake ikazima
chaji kabisa na kujikuta akiidumbukiza mfukoni mwake. Eddy akafika
kwenye chumba alicholazwa Phidaya, akaingia na kukaa pembeni ya kitanda
cha mke wake na kuanza kumtazama usoni mwake, na kuanza kufikiria ni
kitu gani ambacho anaweza kumfanya Mzee Godwin pale atakapo mtia
mikononi
“Sasa huyu mzee amevuka mipaka kwa sasa, nitamuua kimya kimya”
Eddy
alizungumza kwa sauti ya chini kabisa huku akiendelea kumtaza mke wake
kwa macho ya masikitiko. Taratibu akamshika mkono mke wake ambao
haujachomwa sindano ya dripu, taratibu akaubusu kisha akakanyanyuka na
kuanza kupiga hatua taratibu za kuelelea kwenye mlango
Blogger Comment