YALIYOJIRI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akisalimiana na Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzania Bungeni na Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe (MB) wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzania na Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe (MB) akimuuliza swali Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) kuhusu hali ya uchumi nchini ambapo Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa alimhakikishia kuwa Serikali ipo imara katika kusimamia ipasavyo uchumi wa nchi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akijibu maswali ya wabunge wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akiwashukuru wabunge mara baada ya kumaliza kujibu maswali wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Leo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) akijibu swali bungeni ambapo alisema kuwa serikali ipo tayari kushirikiana na raia katika kuhakikisha inakabiliana na biashara haramu ya Madawa ya Kulevya.
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijibu swali bungeni ambapo alisema ambapo alisema Serikali imetenga shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kuboresha Magereza ya watoto pamoja na makao ya Wazee nchini.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba akijibu swali bungeni ambapo alisema serikali ipo katika mazungumzo na serikali ya China kwa ajili ya kuboresha zao la Tumbaku.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akijibu swali bungeni ambapo alisema Wizara imetenga Shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kuboresha hali ya Magereza nchini.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongea na wabunge na kuviasa vyama vya siasa vyenye tabia ya kufukuza wabunge kuacha hivyo kwani hatuwatendei haki wapiga kura na ni gharama kwa serikali.Picha na Hassan Silayo.Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma
Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inaendelea kukutana na wadau tofauti wanaohusika na masuala ya uchumi katika kuhakikisha uchumi wa nchi unaendelea kukua.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe mijini Dodoma aliyetaka kujua hali ya uchumi ilivyo kwa sasa hapa nchini.
Waziri Mkuu amesema kuwa lengo kuu la Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha uchumi wa nchi unaongezeka kupitia nyanja tofauti kwa kushirikiana na taasisi za fedha zilizopo ili kufikia uchumi wa kati kama ilivyoanishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi Akizungumza kuhusu suala la midororo wa upokeaji wa mizigo katika bandari nchini, Waziri Mkuu amesema kuwa mdororo huo umetokana na kupungua kwa kiasi cha mizigo na kushuka kwa uchumi duniani.
Katika suala ya mauaji yaliyotokea Tanga, Mwanza na Vikindu, Waziri Mkuu amesema kuwa usalama wa wananchi utaendelea kuimarishwa huku serikali ikiahidi kupambana vitendo vya mauaji kwa raia na askari katika maeneo mbali mbali nchini.
“Serikali imesikitika sana na jambo hili la mauaji hivyo itahakikisha wauaji hao wanawekwa katika mikono ya Sheria na kuongeza ulinzi kwa maeneo yote nchini kwa kuanzia ngazi ya vitongoji” alifafanua Waziri Mkuu.
Mbali na hayo Waziri Majaliwa ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola katika kuthibiti matukio hayo.
Kuhusu suala la uwepo wa tozo katika zao la korosho swali limeibuliwa na Mbunge wa viti maalumu Mhe.Riziki Lulida (CUF), Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa Serikali imeshatoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusimamia uondoaji wa Tozo zisizo na maana katika zao la korosho.
Blogger Comment