Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kumpa pole kufuatia vifo vya watu na madhara mengine yaliyotokana na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Tetemeko lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, limesababisha vifo vya watu 16, kuacha watu 253 wakiwa na majeraha mbalimbali ya mwili na nyumba zaidi ya 1000 zikiwa zimebomolewa.
Taarifa kutoka kwa msemaji wa Rais Kenyatta, Kenua alisema kuwa Rais Kenyatta ameahidi kutoa msaada wa mabati, blanketi na magodoro ili kuwasaidia watu wasio na makazi mkoani Kagera.
Msaada huo utasafirishwa kwa ndege na Jeshi la Kenya Jumanne Septemba 13 hadi mkoani Kagera ambapo ndipo palipopata madhara.
Blogger Comment