Mtunzi : EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
“Hakikisheni huyu dada nina lala naye usiku wa leo sawa”
Muntar aliwaamrisha wapambe wake na wakamtii na mmoja wao akanyanyuka kwenda kumfatwa Agnes kwenye eneo la kuuzi vinywaji ili kuzungumza ombi la bosi wake analo lihitaji
ENDELEA
“Habari yako dada?”
Kijana wa Muntar alimsalima Agnes ambaya kwa haraka akaliachia tabasamu lake mdomoni na kuufanya uso wake kuzidi kunawiri kwa uzuri
“Salama mamo vipi?” Agnes alizungumza kwa sauti nyororo ya kuvutia hadi muhudumu kiume wa vinywaji akaguna
“Salama.....kwa jina mimi ninaitwa Kibopa na yule pale alavalia cheni nyingi ni bosi wangu anaitwa Muntari”
“Aahaa nashukuru kuwafahamu,Samahani kaka ninaomba unipatie Red’s mbili za baridi kiasi”
“Muhudumu mpe katon nzima pesa nitalipa mimi?”
“Jamani kaka yangu mimi sio mnywaji sana”
“Ahaa usijali nyingine unaweza kunywa leo au hata kesho”
“Asante sana”
Muhudumu akamkabidhi Agnes katoni ya kinywaji alicho muagizia na kibopa akatoa pesa na kumlipia muhudumu.
“Sasa sister kama huto jali ninaomba namba yako ya simu”
Agnes bila wasiwasi akamtajia Kibopa namba yake ya simu,wakaagana ana Agnes akarudi sehemu alipo Rahab
“Jamaa ameshaingia mkenge sasa kazi ni moja sawa”
“Hapo ndipo ninakupendea Ag”
“Chezea mimi wewe,kumbe mtu ukiwa na kalio kubwa nalo linasaidia”
Wakacheka na kufungua vinywaji na kuanza kunywa taratibu.Muntar akakabidhiwa namba na Kibopa na akaipiga na Agenes akaipokea na kama kawaida na sauti yake nyororo aliyobarikiwa kutoka mbinguni akazungumza
“Nani mwenzangu?”
“Ukigeuka upande wako wa kushoto utaniona nimevaa shati jeupe na cheni za dhahabu”
Agnes akageuka na kumfanya Muntar kupunga mkono akimuashiria kuwa ni yeye ndiye aliye mpigia simu
“Mrembo nakuomba basi uje kujumuika name hapa?”
“Naona aibu labda nije na mwezangu”
“Hilo tuu hakuna tatizo ni wewe tuu”
“Sawa ninakuja”
Agnes akakata simu na kumtazama Rahab kwa pamoja wakatabasamu na wakasimama na kuanza kutembea kwa mwendo wa maringo na kupishwaviti na wapambe wa Muntar kisha wakakaa
***
Dokta Wiliama akawashusha kwenye gari Anna,Halima na Fety mbali kidogo na hotel ya Serena huku kila mmoja simu yake ikiwa na salio la kutosha pamoja na picha ya Karim Yussuf kijana mwenye umri mdogo ila anasifika sana kuwa na utajiri mkubwa kutokana na Sheli za mafuta anazo zimiliki kila kona ya mikoa ya Tanzania.Kila mmoja akaingia Hotelini kwa muda wake na kuelekea kuketi katika upande wake ila kwa pamoja wakawa na mawasiliano ya ujumbe mfupi wa meseji.Kutokana ni muda wa jioni hawakuwa na papara kwani watu wengi bado hawakuwa wameingia Hotelini kuendelea na starehe zao.Macho ya Fety yakatua kwa jamaa anayeingia kwenye mlango wa kuingilia akiwa ameongozana na mwanamke mrembo
{Nimemuona}
Fety akausamba ujumbe kwa wezake ambao wapo maeneo ya tofauti kwenye hoteli na taratibu simu yake akaichomeka kwenye suruali yake na kuendelea kumtazama Karim ambaye moja kwa moja aka anaelekea sehemu yenye milango ya lifti zinazo kwenda juu na kushuka chini,Kutokan-a na Lifti kutumika ikamlazimu Karimu na mpenzi wake kusimama kwa muda kuzisubiria.
Kwa haraka Fety akasimama na kupiga hatua za haraka kabla hajafika sehemu alipo Karimu,lifti ambayo wanaisubiria ikafunguaka,Karim na mpenzi wake wakingia ila kabla haijajifunga Fety akawahi kuizuia na kuingia
“Habari zenu?”
“Salma”
Karimu kutokana na kutokuwa na aibu akaanza kumshika shika mpenzi wake na kuchezeana katika sehemu zao nyeti.Mcho ya Fety yakawangalia kwa umakini kisha akayahamishia masho yake kwenye kamera mbili za ulinzi zilizopo ndani ya lifti kabla hajafanya kitu chochote akastukia lifti ikisimama hii ni baada ya mpenzi wa Karimu kuminya kitufe cha kuisimamisha lifti.
Kufuma na kufumbua Fety akastukia ngumi kutoka kwa mpenzi wa Karim ikitua kwenye shavu lake na kumsfanya kuweweseka kasha akaanza kuikwepa mikono inayoimjia mwilini mwake kutoka kwa Karimu na mpenzi wake Shamsa mwenye asili ya kiarabu.
Blogger Comment