MWANAMKE AKIRI KUMUUA MUME WAKE KISA USALITI.


Hili linaweza kuwa moja ya matukio ya kushangaza kama sio kusikitisha, mwanamke mmoja nchini Kenya aliamua kukodisha kundi la watu wamtoe uhai mume wake baada ya kugundua ana uhusiano na mwanamke mwingine.


Mwanamke aitwaye Faith Wairimu amekiri kumkodishia mume wake John Muthee ambaye wameishi kwa miaka 15 kundi la watu wa kumuua huko Nairobi Kenya wiki hii.Kwa mujibu wa mtandao wa Standard Digital, maafisa uchunguzi wameieleza mahakama kuwa Wairimu alitafuta watu alioelewana nao kuwalipa shilingi ya Kenya 200,000 na kuwatangulizia Ksh 40,000 kwa makubaliano ya kuwamalizia kiasi kilichobaki baada ya kazi ambapo walitakiwa kumletea nguo za mumwe wake zikiwa zimeloa damu kama uthibitisho (mission accomplished).
Imefahamika mahakamani hapo kuwa hili lilikuwa ni jaribio la mara ya pili la mama huyo mfanya biashara wa kiosk kutaka kumuua mumewe baada ya jaribio la kwanza kugonga mwamba.
Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka Karuri Thuku, mwanamke huyo alitaka kumuua mume wake baada ya kugundua alikuwa na mahusiano na mwanamke mwingine aitwaye Njeri Wambaa.
Tukio kamili:
Thuku aliieleza mahakama kuwa Faith alimtafuta mwanamke mmoja aitwaye Mama Kevo na kumpa kibarua cha kutafuta kundi la wanaume watakaotekeleza ukatili huo wa mauaji ya Muthee. Mama Kevo naye alianza kibarua chake kwa kumtafuta mtu mwingine wa kumsaidia kupata watu wa kazi hiyo (inavyoonekana haikuwa rahisi kuwapata).
Mama Kevo alipata mtu wa kumuunganishia kwa wazee wa kazi hiyo aitwaye Wilson Mwangi bila kujua kuwa mtu aliyempata ni ‘police informer’ na ndipo negative ya mkanda huo ilipoanza kuingiwa na giza.
Baada ya Mwangi kuachana na Mama Kevo alipiga simu polisi na kuripoti juu ya mpango wa mama huyo na aliyemtuma kutaka kumuua mume wake.
Kilichotokea baada ya taarifa kufika polisi ni kama ambavyo huwa tunaona katika movie, polisi walitengeneza mtego kwa kutuma maaskari watatu kwenda na Mwangi kwa Mama Kevo ili wajidai kuwa ndio watu waliopatikana kwaajili ya kazi moja tu ya kumwaga damu ya Muthee.
Baada ya Mama Kevo kuwatambulisha wahusika walienda kuonana na Wairimu kesho yake katika kiosk chake, ndipo alipofunguka kwao kuwa anahitaji wamuhakikishie kuwa hawatashindwa kumuondoa mume wake kama ilivyokuwa katika jaribio lake la mwanzo (siri ya zamani ikawa imefichuka). Mmoja wa Maaskari hao (ambao hakuwajua) alimuonesha bastola kumthibitishia wamejiandaa vizuri kwa kazi.
Baada ya makubaliano yaliyofanyika (June 17) Wairimu aliwalipa kianzio cha 40,000 Ksh kwa m-pesa na kubaki akidaiwa 160,000 ambazo zilipangwa kulipwa baada ya kazi kukamilika na kisha akawapatia namba ya mume wake ili waanze utekelezaji.
Baada ya maafisa hao wa polisi kumpigia Muthee wakijifanya kuwa wateja (sababu ni mfanya biashara) ili atoke nyumbani kwake kama walivyoelekezwa na (bosi wao) Waimuri lakini ilishindikana sababu hakutoka siku hiyo.
Jumanne ya wiki hii (June 18) mtuhumiwa aliwapigia maaskari hao ambao alkuwa bado anaamini kuwa ni watu watakaomuua mume wake na kuwataarifu kuwa anaongozana na mume wake na akawaelekeza mahali walipo.
Baada ya mama huyo kuwaona wauaji wako karibu alisogea pembeni mita chache ili awape nafasi ya kulenga vizuri, lakini maaskari hao walimkamata Muthee na kwenda naye mpaka kituo cha polisi kule ambako mpango wa kumuwekea mtego Wairimu ulikopangwa na wakampigia Wairimu kumpa taarifa kuwa tayari wamemuua mume wake.
Afisa mmoja wa polisi alichukua jaketi la MUthee na kulipitisha katika bucha moja ya jirani kwaajili ya kulipaka damu kisha akampelekea Wairimu kama uthibitisho kama walivyokubaliana na akamalizia pesa waliyokuwa wamekubalaiana 160,000 kisha wakamkamata.
Katika utetezi wake wairimu alikiri kuwa ni kweli alikusudia kumuua mume wake kutokana na matatizo ya muda mrefu ya kifamilia na usaliti wa mume wake, “It is true I conspired to kill him because he has been beating me and not paying school fees for the children. I am everything in the house; his only work is to drink and move around with other women,” Alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment