Kompyuta mpakato zenye majibu ya watu waliopima ukimwi pamoja na majina yao zimeibwa mkoani Tabora.
Kompyuta hizo zipatazo 30 zenye thamani ya Sh70 milioni, zimeibwa kwenye ofisi ya shirika lisilo la kiserikali la Jhpiego linaloshughulika na masuala ya Ukimwi na tohara.
Kompyuta hizo zimeibwa mwishoni mwa wiki kwenye ofisi hiyo iliyo jirani na ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa amesema tayari taarifa za tukio hilo zimewafikia na wanaendelea na uchunguzi wa kina kufahamu kilichotokea.
Inadaiwa kuwa kompyuta hizo, zina majina ya watu waliopima VVU na majibu yao.
“Kinachotatiza ni kwamba kama majina ya watu wenye virusi yakijulikana itakuwa ni utata mkubwa kwani ofisi hiyo itakuwa imewaweka katika wakati mgumu pasipo wao kupenda,” kilisema chanzo chetu cha habari.
Mkurugenzi wa Jhipego, Dk Albert Komba amethibitisha kutokea kwa wizi huo.
Blogger Comment