Wanaswa na dawa za kulevya Ilemela-Mwanza



Mkuu wa wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dk Leonard Masale amesema watu 94 katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, wamekamatwa katika kipindi cha mwaka 2015/16, wakijihusisha na biashara ya dawa za kulevya aina ya bangi, heroin na mirungi. Alisema hayo alipokuwa akisoma risala ya utii ya wananchi wa Ilemela kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
Dk Masale alisema uongozi wa wilaya na manispaa, unaendelea kutoa huduma rafiki kwa waathirika wa dawa za kulevya kwa kushirikiana na kituo kinachotoa huduma kwa waathirika na lengo ni kumaliza tatizo hilo.
Katika mapambano dhidi ya rushwa, Dk Masale alisema katika kipindi hicho, Serikali kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ilichunguza malalamiko 21 na kuwakamata watu watano kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.
“Kesi tatu za rushwa ziko mahakamani. Jumla ya watu 2,474 wamepata elimu dhidi ya madhara ya rushwa kwa njia mbalimbali, ikiwemo semina 8, mikutano ya hadhara 7, maonesho 2 na vipindi vya redio 8 kwa mwaka 2015,” alifafanua.
Alisema klabu za wapinga rushwa 18 katika shule za msingi, sekondari na vyuo zimefunguliwa kutoa elimu juu ya madhara ya rushwa kwa wananchi.
Alisema katika kipindi hicho, wilaya ilitoa mkopo wa Sh 50, 201, 200 kwa vikundi 20 vya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi ili kuvijengea uwezo wa kiuchumi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment