Katika kuhakikisha wanaboresha mashindano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA Champions League), Chama cha Soka Ulaya (UEFA) limepanga kufanya maboresho ya idadi ya timu ambazo zitakuwa zinafuzu ili kuhakikisha zinapita timu bora.
Mabadiliko hayo ni kuchukua moja kwa moja timu nne kutoka katika ligi nne bora barani humo kuingia katika hatua ya makundi tofauti na sasa ambapo mataifa yote timu inayoshika nafasi ya nne katika ligi yao inacheza kwanza michezo ya awali ili kupata nafasi ya kutinga hatua ya makundi.
Mpango huo umekuja baada ya Kamati ya Mashindano ya UEFA kukutana kujadili ni jinsi gani watazifanya ligi kubwa Ulaya zinasalia kuwa ligi bora na timu zao zipate nafasi kubwa ya kushiriki ligi ya mabingwa tofauti na vilabu ligi zingine.
Mabadiliko hayo yatazihusisha timu zinazotoka ligi nne bora Ulaya ambazo ni Uingereza, Ujerumani, Hispania na Italia.
Blogger Comment