SOMA KISHA TAZAMA VIDEO: SINTOFAHAMU YA VYAMA VYA SIASA INATATULIWA KWA KUKAA NA KUZUNGUMZA PAMOJA-JAJI MUTUNGI


MSAJILI wa vyama vya Siasa nchini, Jaji Mstaafu, Francis Mutungi 
Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii.
MSAJILI wa vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema masuala yote ya  sintofahamu kwa vyama vya siasa yatatuliwa katika meza ya majadiliano na si vinginevyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Jaji Mutungi amesema kuwa kuna taharuki au hofu ambayo inajengwa kwa wadau wa siasa ambayo inahitaji kuwepo mazungumzo kutokana na taratibu zinazohusu utawala bora.
Amesema kuwa utawala bora ni kuheshimu miundombinu iliyowekwa kwa kufuata sheria zake na bila kufanya hivyo miundombinu haitakuwa imetendewa haki kwa watu kufanya chochote bila kuangalia misingi iliyowekwa katika miundombinu hiyo.
Amesema kuwa Baraza la vyama vya siasa limeandaa mkutano wa wadau wa vyama vya siasa pamoja na watu wengine kuweza kuzungumza masuala mbalimbali ambayo yamejitokeza katika kipindi hiki na kupatiwa ufumbuzi wa sintofahamu miongoni mwa  wadau.
Jaji Mutungi amesema kuwa baraza la vyama vya siasa linatarajia kukaa  Agosti 29 na 30 kutaka wadau wote waweze kushiriki ili kutafuta suluhu kwa yale ambayo yamejitokeza sambamba na kuyatafutia suluhu katika kuendelea kulinda amani ya nchi yetu.
Amesema  siku zote watu wanatafuta mwafaka wa jambo lolote katika meza ya mazungumzo na kupata suluhu katika kulinda amani ya nchi yetu.

Aidha amesema suala la Chama cha Wananchi (CUF) anaangalia na kuona jinsi gani anaweza kushauri kutokana na kuwa mlezi wa vyama vyote ambavyo vimepata usajili katika ofisi yake.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment