Sakata la Jaribio la Kumpindua Rais wa Uturuki Lachukua Sura Mpya

Erdogan-2Waziri Mkuu wa Uturuki, amesema zaidi ya watu 40,000 wanashikiliwa na Polisi wakihusishwa na jaribio la kutaka kuipindua Serikali ya rais wa nchi hiyo, Erdogan.
Katika hotuba yake ya moja kwa moja katika Televisheni, Binali Yildirim pia alisema takriban wafanyakazi wa sekta ya Umma 80,000 wamefutwa kazi wakiwemo wanajeshi, Polisi na watumishi wa Umma.
Maelfu ya Taasisi yameshukiwa kuwa na mahusiano na Kiongozi wa kidini, Fethullah Gulen zimefungwa.
Serikali ya Uturuki imemshutumu Gulen, ambaye anaishi uhamishoni nchini Marekani kwa kusuka mipango ya mapinduzi .
Awali, Serikali ya Uturuki ilisema itawaachia huru watu 30,000 ili kupunguza mrundikano kwenye magereza.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment