Sababu za TAKUKURU Kumkamata Rais wa Simba Evans Aveva

Asubuhi ya August 4 2016 taarifa zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na Rais wa Simba Evans Aveva kutiwa mikononi mwa Polisi kutokana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuagizwa kukamatwa kwa kiongozi huyo. millardayo.com ilifanikiwa kumpata kaimu afisa msemaji wa TAKUKURU Tunu Mleli na kuweka wazi.

“Ni kweli Aveva amekamatwa na polisi baada ya TAKUKURU kuagiza hivyo kutokana na tuhuma za rushwa zinazomkabili, tuhuma zinazomkabili ni uchepushwaji wa fedha kutoka account ya Simba kwenda katika account yake na baadae kuanza kufanyiwa mgawanyo katika account nyingine, ni fedha za usajili wa Okwi kutoka Etoile du Sahel”

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment