Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeongeza nguvu kwa kutuma askari wengine 80 katika oparesheni ya kusaka majambazi inayoendelea katika maeneo ya Vikindu, wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Akizungumza na vyombo vya habari leo katika kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo Kamishna Simon Sirro, amesema Jeshi hilo limeanza rasmi oparesheni hiyo usiku wa kuamkia jana, ikiwa na lengo la kusaka watu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi wanaodaiwa kufanya matukio kadhaa ya ujambazi likiwemo lile la kuuawa kwa askari wanne waliokuwa wakienda lindoni, katika benk ya CRDB, Mbade jiji Dar es Salaam.
Amesema kuwa katika oparesheni hiyo kuna watu waliouawa na wengine wanashikiliwa na jeshi hilo, lakini amekataa kutaja idadi yoyote ile ya waliouawa au waliokamatwa kwa sababu za kiusalama kwa kuwa oparesheni hiyo bado inaendelea.
“Itakuwa ni kinyume cha utaratibu nikieleza kinachoendelea kwenye operesheni, niwahakikishie silaha zilizochukuliwa zinarudi,kinachoendelea nitawajulisha jumanne ili wananchi wajue kitu gani kinaendelea,” amesema.
Ameongeza kuwa; “Mapambano ni ya kawaida sana, na ndio maana askari polisi akifa kwa silaha ni jambo la kawaida sana. Operesheni tutaifanya maeneo ya Vikindu, Pwani Dar es Salaam, sababu hii network (mtandao) ipo na lazima tutaisafisha.Kama walidhani wataitawala DSM wamejidanyanya lazima tutarudisha heshima ya jiji.”
Katika hatua nyingine, Sirro amesema amepata taarifa kuwa wapo baadhi ya watu wanapewa fedha kwa ajili ya kufanya maandamano Septemba Mosi mwaka huu ambapo ametoa onyo kwa watakaoshiriki kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kuwa maandamano hayo hayajaruhusiwa.
“Wote tunajua madhara ya fujo, wazalendo naomba msishiriki, Wanaotaka kujionesha wanapambana na polisi waje barabarani, ”amesema.
Usiku wa kuamkia jana, hali ya taharuki iliwakumba wakazi wa Vikindu baada ya kikosi maalum cha askari kuvamia nyumba moja iliyoko eneo hilo, na kisha kuzuka kwa majibizano ya risasi kati ya polisi na wanaodaiwa kuwa ni majambazi waliokuwa katika nyumba hiyo.
Baadhi ya askari wakiwa tayari kwenye magari yao wakati wa kujiandaa kuelekea Vikindu kwenye mapambano
Vikosi hivyo vikitoka makao makuu ya kanda maalum ya Dar kuelekea kwenye mapamban
Blogger Comment