Ndugai atua Dodoma Atoa Kauli nzito

Image result for Job Ndugai

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amesema uamuzi wa serikali kuhamia makao makuu Dodoma, ambao ulitamkwa na Rais John Magufuli kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wao kama Bunge kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya kazi Dodoma na makao makuu ya taasisi ya Bunge yako Dodoma.
Alisema kwa kuwa uamuzi huo umefanyika, watumishi karibu wote wa Bunge watahamia Dodoma na Dar es Salaam watabaki watumishi wachache kwa ajili ya huduma maalumu. “Bunge litaanza kufanya shughuli Dodoma kwa asilimia zote mia kwa shughuli za Kamati na vikao vya Bunge zima,” alieleza.
Alipohojiwa suala la Ukawa katika vikao vya Bunge na kutokuwa na imani na Naibu Spika na maspika wastaafu kufanya usuluhishi ili kupata muafaka, Ndugai alisema, “Ndio nawasili, wabunge wenzangu wanaanza kuwasili, nina hakika timu itakapokamilika wabunge wote wakiwa wamekamilika wa CCM na upinzani, nina hakika tutatafuta njia ya kufanya kazi kwa pamoja.”
Alisema kinachomgusa, si suala la wabunge wa upinzani kutoka nje, kwani hilo ni jambo la kawaida, au la mbunge mmoja mmoja anasaini anatoka, kwani kuna wabunge hata wa CCM waliokuwa wakitoka nje kivyao. Lakini, alisema shida kubwa anayoiona ni wabunge kutokuwa na mahusiano mazuri, kati ya wale wa CCM na wa Upinzani.
“Tatizo langu mimi ningependa tuelewane na wabunge, ilifikia mahali mahusiano ya wabunge wa pande hizi mbili yalikuwa mabaya mno, kama mnakumbuka sehemu kubwa ya kipindi kile kilikuwa ni mwezi wa Ramadhani, ilifika mahali hata mtu fulani akitengeneza futari watu wa upande fulani hawawezi kwenda kula futari ile,” alisema Ndugai ambaye kwa muda mrefu hakuwapo katika uongozi wa mhimili huo wa Dola, akiwa India kwa matibabu.
Pia alisema wengine hawasalimiani, wakawa na uadui, wengine wanaenda kanisa moja au msikiti moja, wakitoka pale hawasalimiani. Mbunge anasalimia watu wengine na hamsalimii mbunge mwenzake, anamuacha katika mazingira hayo ya chuki kubwa kiasi hicho.
Alisema hayo mazingira hayapendezi, wabunge ni timu moja na ushirikiano katika kazi ni lazima ujengwe na udumishwe. 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment