CHADEMA YAPATA PIGO...HATI YA KIFO KUCHUNGUZWA

Image result for CHADEMA
HAKIMU Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage, ameutaka upande wa Jamhuri, kuchunguza hati ya kifo cha Raia wa Angola, Jose Nimi aliyekuwa anakabiliwa na mashitaka ya kukusanya matokeo na kuyachapisha kupitia mitandao ya kijamii bila ya kuihusisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Mwijage alitoa agizo hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, baada ya mdhamini wa mshtakiwa wa saba, Mfuime Sapi kuwasilisha mahakamani hapo cheti cha kifo cha mshtakiwa huyo. Kwa mujibu wa taarifa hizo, inadaiwa Nimi alifariki Dunia Juni 20 mwaka huu katika Hospitali ya Sinza, Dar es Salaam.
Hakimu Mwijage alisema Mahakama imepokea cheti hicho pia imemuondoa Nimi katika kesi hiyo, lakini upande wa Serikali unatakiwa ufanye uchunguzi kuhusu taarifa hizo na kujiridhisha kama kweli mshtakiwa huyo amefariki. Wakili wa Serikali, Salim Msemo alikubali agizo lililotolewa na kuhakiki cheti hicho kwa kufanya uchunguzi.
Kesi hiyo itatajwa Septemba 15 mwaka huu. Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mashinda Mtei (45), Julius Mwita (30), Frederick Fussi (25), Meshack Mlawa (27), Anisa Rulanyaga (41) na Julius Matei (45).
Inadaiwa washtakiwa walifanya makosa hayo, kati ya Oktoba 25 na 26 mwaka jana katika maeneo tofauti, Dar es Salaam, kupitia mtandao wa kitaifa wa usimamizi wa uchaguzi uliopewa jina la “Mfumo wa usimamizi wa matokeo ya uchaguzi wa M4C” (M4C National Results Management System) na mitandao mengine ya kijamii ya Facebook na Twitter.
Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo, baada ya kufahamika kuwa data walizoweka mitandaoni hazikuwa sahihi na hazikuwa na ukweli wowote, ambapo zilidaiwa zinapotosha umma juu ya matokeo yaliyokuwa yanaendelea kutolewa na NEC.
Aidha Matei na Nimi wanadaiwa kujihusisha na ajira bila kibali siku ya Oktoba 26 mwaka jana , wakiwa katika Hotel ya King D iliyopo wilaya ya Kinondoni wakiwa na vitambulisho vya uraia wa Kenya na Angola vyenye namba A.1532119, 30879 na M.27687807 wakishiriki katika ajira ya kukusanya na kuchapisha matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa Chadema bila ya uhalali wa kibali.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment