Hivi karibuni Rais Magufuli katika ziara yake mkoani Mwanza aliwaonya walimu wanaotoa taarifa za uongo za wanafunzi ili kujipatia fedha nyingi za elimu bure. Sasa wilaya ya Kinondoni Dar es salaam imefanya ukaguzi kwa shule za msingi na sekondari ambapo imebaini wanafunzi 3462 katika shule za msingi 68 na 2534 katika shule za sekondari 22 ambao hawajaandikishwa kwenye kitabu cha takwimu na wamebainika kutokuwa na sifa za kupata ruzuku hizo.
Baada ya kubaini mapungufu hayo Mkuu wa wilaya Ally Hapi amemuagiza mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kuwavua madaraka wakuu wa shule za msingi 68, pamoja na kumuandikia barua Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwavua vyeo wakuu wa shule za sekondari 22 baada ya kubaini kuna wanafunzi hewa zaidi ya 5000 katika shule za msingi na sekondari katika manispaa hiyo………..
>>>’Wamefanya udanganyifu kwa maslahi yao binafsi kufuatia hilo mkurugenzi wa manispaa atawavua madaraka wakuu wa shule za msingi waliofanya udanganyifu’:-Ally Hapi
>>>’Serikali kila mwezi inapoteza Bilioni 18.8 kwa ajili ya kugharamia elimu bure hivyo udanganyifu uliofanywa ni ukosefu wa maadili na uzalendo’:-Ally Hapi
Blogger Comment