Yanga yapigwa mvua ya magoli

CAF Preview: Medeama vs Yanga , Jangwani mguu nje mguu ndani
YANGA jana ilizidi kujiweka pagumu kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Medeama ya Ghana.
Hiyo ni mechi ya nne kwa Yanga inacheza bila kupata ushindi huku timu nyingine kwenye kundi hilo zikishinda baadhi ya mechi zake.
Yanga ilipoteza kwa bao 1-0 katika mechi mbili dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria na TP Mazembe ya Congo DR kisha ikatoka sare ya bao 1-1 na Medeama katika mechi ya kwanza nyumbani na jana ikapoteza mechi ya marudiano na timu hiyo.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Sekondi Takoradi, Yanga ilionekana kuzidiwa tangu mwanzo wa kipindi cha kwanza huku beki wake namba nne na tano wakionekana kupoteana. Medeama ilipata bao lake la kwanza mapema katika dakika ya saba likifungwa na Daniel Amoah baada ya kuunganisha mpira wa kona.
Wenyeji hao walipata penalti katika dakika ya tisa lakini kipa wa Yanga, Deogratius Munish ‘Dida’ alipangua mkwaju huo. Mwamuzi alitoa penalti hiyo baada ya nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kumfanyia madhambi mchezaji wa Medeama.
Dakika ya 23, Medeama ilipata bao la pili likifungwa na Abbas Mohammed na dakika mbili baadaye Simon Msuva aliifungia Yanga bao lake la kwanza kwa mkwaju wa penalti.
Medeama aliyoonekana kucheza kwa kasi mchezo huo kwa karibu dakika zote za kipindi cha kwanza, waliandika bao la tatu katika dakika ya 37 kupitia kwa mfungaji wa bao la pili, Mohammed. Kipindi cha pili hakikuwa na kasi sana na Yanga walionekana kubadilika kiasi licha ya wenyeji wao kuwapa mashambulizi ya kushtukiza.
Kwa matokeo hayo, Yanga imeendelea kushika mkia kwenye kundi A ikiwa na pointi moja, huku Medeama ikifikisha pointi tano sawa na Mo Bejaia ya Algeria, inayocheza na vinara wa kundi hilo TP Mazembe ya Congo DR wenye pointi saba leo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment