

Tamasha la Sauti za Busara limo kwenye matasha 25 bora ya kimataifa na mtandao wa kitalii wa Afro Tourism’s umeliingiza tamasha hili katika matasha 8 bora ya muziki. Na mwezi wa Februari 2015, BBC World Service imelitaja tamasha la Sauti za Busara kama ni ‘moja kati ya matukio muhimu na yenye kuheshimika barani Afrika.
TAMASHA la Sauti za Busara ni miongoni mwa machache ambayo yamejenga historia kutokana na kuutangaza na kuuendeleza muziki wa Tanzania nje ya mipaka yake, ambako mwaka huu limeanza toka juzi jumapili July 10, 2016 na hivi sasa linaendelea.
KATI ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya saba kutoka Dar es Salaam na watatu kutoka Uganda ambao video zao zinashindanishwa kupata moja yenye mpangilio mzuri wa hadithi za filamu, atakuwa balozi wa Ziff kwa mwaka huu.
Mkurugenzi wa Tamasha la 19 la Kimataifa la Filamu Nchi za Jahazi (Ziff), Profesa Mhando, alisema kwamba wamepanga kumpata balozi mmoja wa tamasha hilo kutokana na video za wasanii hao watakaowashindanisha ili kuleta hamasa ya ukuaji wa video za muziki nchini.
“Video itakayochaguliwa kuwa bora na majaji wetu, tutamtangaza msanii wa video hiyo kuwa balozi wetu, tutakuwa tukimlipa kwa mwaka mzima na atatunga na kurekodi wimbo wa Ziff kwa tamasha lijalo,” alisema Profesa Mhando.
Alisema video hizo zilipatikana baada ya kutangaza kupokea video watakazozishindanisha wasanii wa muziki.
“Tulitangaza walete kazi zao na wachache wameshaleta na atakayeshinda ndiye tunatarajia awe balozi wetu na kuleta hamasa kwa wasanii wengine kuleta kazi zao kwa tamasha la mwakani ambalo litakuwa maalumu kwa kuwa linatimiza kuwa tamasha la 20,” alisema.
Baadhi ya video zitakazoshindanishwa ni pamoja na ‘Aje’ wa Ali Kiba, ‘Sweet sweet’ wa Chege Chigunda, ‘Zigo Remix’ wa Ay aliomshirikisha Diamond Platnumz na ‘Sizonje’ wa Mrisho Mpoto.
Blogger Comment