Jokate uvumilivu umenishinda

jokate12
DAR ES SALAAM: Mwanamitindo ‘the big name Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ameibuka na kusema kuwa uvumilivu alionao na kujichanganya na watu unakaribia kumshinda kwa sababu unawapa nafasi kumtukana mitandaoni hivyo anawaonya kwani amechoshwa na hali hiyo.
Akizungumza na Wikienda, Jokate alifunguka kuwa anachukizwa na watu wanaotukana wenzao mitandaoni ndiyo maana uvumilivu ulimshinda na kujikuta akimtolea uvivu mtu aliyekibeza kidoti chake, akamjibu ndivyo sivyo.
“Unajua tunawapenda sana mashabiki wetu lakini kuna wakati wanatukosea, unakuta mtu ametoka alipotoka anakukomentia kitu ambacho siyo, kiukweli sitakubali kutukanwa, mimi ni mpole lakini sipendi upole wangu unifanye kutukanwa tu, nitachukua hatua,” alisema Jokate.
Hivi karibuni Jokate alitupia picha yake mtandaoni ya pozi la uso ambapo mtu mmoja akamuuliza kama ni kidoti au upele ndipo alipompa jina ambalo lilionekana ni tusi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment