WATUMISHI WA AFYA SASA HAPATOSHI;Namba za Simu za Utoaji Wa Malalamiko Na Kero Juu Ya Huduma Za Afya Nchini Pamoja Na Masuala Ya Jinsia, Wazee Na Watoto Zatolewa

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inayo dhamana ya kusimamia na kuratibu Mipango, Sera, Sheria na Mikakati mbalimbali inayolenga kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini pamoja na kujenga jamii ya watanzania inayojali na kuheshimu Usawa wa Jinsia, Haki za Wazee na Watoto.

Katika utekelezaji huu, yapo mafanikio kadhaa yaliyopatikana lakini pia zipo changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utoaji wa huduma za afya hapa nchini. Baadhi ya changomoto hizo ni za kiutendaji zaidi ambazo zinaweza kutatuliwa kwa haraka endapo tutaimarisha usimamizi na uwajibikaji katika kila ngazi kuanzia ngazi ya Wizara, Mikoa, Wilaya na Vituo vya kutolea huduma za afya. Changamoto hizi ni pamoja na wagonjwa kutopatiwa huduma haraka na sahihi, lugha na kauli mbaya kutoka kwa watoa huduma na makundi yanayotakiwa kupata matibabu bure (yaani Wazee, Wajawazito na Watoto wa umri wa chini ya miaka 5) kutozwa fedha kinyume na Sera ya Afya ya 2007)

Takribani kila siku vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti matukio kadhaa kuhusu malalamiko na kero mbalimbali wanazokumbana nazo wananchi katika kupata huduma za afya. 

Wasimamizi wa Wakuu wa Utekelezaji wa Sera na Miongozo ya Afya katika ngazi ya Mikoa ni Waganga Wakuu wa Mikoa. Ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya pamoja na kuhakikisha malalamiko na kero zao zinashughuhulikiwa kwa haraka, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) ameamua kuweka wazi namba za simu za Waganga Wakuu wa Mikoa (RMO) wote nchini ili wananchi wanapokuwa na malalamiko/kero waweze kuwasiliana nao moja kwa moja. 


Mhe Waziri amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa kuyafanyia kazi masuala yote yanayoletwa na wananchi katika Mikoa yao na kuyapatia ufumbuzi haraka. Hivyo, wananchi wasisite kuwasiliana nao kupitia namba zao zifuatazo pamoja na kwa barua pepe.

Katika muktadha mzima wa kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa Sheria na Sera za Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini, mwananchi yoyote ambae ana malalamiko, maoni au ushauri kuhusu sekta husika unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu (Mb) kupitia simu namba 0746 – 505030 (kwa njia ya ujumbe) pamoja na kueleza mkoa uliopo, twitter @wamjw na email: waziri@moh.go.tz

  
“Uwazi na Uwajibikaji ni chachu ya kuleta mabadiliko katika sekta ya afya, sambamba na kulinda Haki za Watoto, Wazee na Wanawake”.

MAWASILIANO NA WAGANGA WAKUU WA MIKOA (RMOs)

IMETOLEWA TAREHE 22/08/2016
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment