Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo |
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limewaonya wananchi kutofanya vurugu za aina yoyote ambazo zinadaiwa kuratibiwa na kikundi cha watu.
Akizungumza na waandishi habari jana, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema taarifa za kiintelejinsia pamoja na vyanzo mbalimbali vya habari zimebaini kuwa kuna kikundi cha watu kinajipanga kufanya vurugu siku za usoni.
“Kuna baadhi ya watu na vikundi vya watu vinaratibu kufanya vurugu siku za mbele wakati wananchi wamejikita katika shughuli mbalimbali za maendeleo na uzalishaji, nitumie fursa hii kuwaonya watu ama vikundi hivyo kuacha tabia hiyo mara moja,” alisema.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi wa mkoa wa Arusha kutojiingiza katika makundi hayo yanayotaka kuvuruga amani na utulivu uliopo katika mkoa wa Arusha.
Kwa mujibu wa Mkumbo, mtu yeyote anayehisi kuonewa afuate taratibu za kisheria katika kudai kudai haki na sio kuwaingiza wananchi katika machafuko.
Blogger Comment