JK: Haikuwa rahisi kumshawishi JPM kuwa Mwenyekiti wa CCM

Mwenyekiti wa CCM anayemaliza muda wake anasema kuwa alitumia kila aina ya ushawishi ili Magufuli akubali kumpokea kijiti kabla ya Novemba 2017. Anasema kuwa alimuendea Ikulu kumshawishi ampokee kijiti. Hata hivyo, Rais Magufuli alimjibu kuwa ana mambo mengi ya kushughulikia ndani ya CCM hivyo haoni kuwa ni muda muafaka wa yeye kubeba dhamana ya kuwa Mwenyekiti wa CCM. Kikwete anasema kuwa pamoja na maelezo yake ya kina, hakika Magufuli hakukubali kubeba dhamana hiyo. Mwisho na kwa lengo la kukata mazungumzo hayo, Rais Magufuli alimkaribisha ugali na hivyo jitihada zake zikagonga mwamba.

Anasema kuwa kutokana na hali hiyo, alimtuma Makamu Mwenyekiti Philip Mangula akamshawishi Rais kwani uzee ni dawa. Baada ya mwezi na nusu, Mangula akarudisha jibu kuwa Rais amekubali kuwa Mwenyekiti wa CCM na ndipo tarehe ikapangwa.

Kikwete anasema kuwa hata yeye alimkatalia mzee Mkapa mwaka 2006 kwa sababu kama hizo hizo ambazo. Hata hivyo anasema kuwa tofauti na 2006 ambapo hakukuwa na magazeti chonganishi na mitandao ya kijamii, mwaka huu wamemtungia uongo kuwa eti yeye anang’ang’ania madaraka na kwamba hataki kumkabidhi madaraka Magufuli. Shabaha yao ni kuchochea mfarakano na baada ya kuona CCM ni moja. Anawaomba wana CCM kuwa wamoja kwa vile wapinzani wao kila wanachokamata hakikamatiki.

Anasema kuwa kama angekuwa hataki kuachia nafasi, baada ya awali Rais kusema kuwa hana haraka ya kuwa mwenyekiti wa CCM, asingemtuma mzee Mangula. Aliamua kumtuma mzee Mangula kutokana na umuhimu wa kofia mbili kwa chama na serikali. Anasema kuwa mfumo huu wa kofia mbili una faida kubwa kwa chama na walioasisi mfumo huu waliona mbali. Anasema kuwa yeye hakutaka guu lake liote tende kwa kufanya maamuzi ya kutenganisha kofia.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment