HUKUMU ya kesi ya mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi imeahirishwa hadi Julai 25.

HUKUMU ya kesi ya mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi inayomkabili askari Polisi, Pacificius Simoni iliyokuwa itolewe jana katika Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa, imeahirishwa hadi Julai 25.
Akiahirisha hukumu hiyo, Kaimu Msajili wa Mahakama hiyo, Jofrey Isaya, alisema inaahirishwa kwa sababu Jaji Paulo Kiwehlo, aliyekuwa akiisikiliza yuko nje ya Iringa kwa majukumu mengine ya kikazi.
Jana katika eneo la Mahakama, nje na ndani, ulinzi uliimarishwa zaidi ya siku nyingine kesi hiyo ilipokuja kutajwa.
Mamia ya wananchi akiwemo Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deo Nsokolo, walionekana mahakamani hapo kufuatilia hukumu hiyo.
Mtuhumiwa kwa mara ya kwanza alifikishwa mahakamani hapo Septemba 12, 2012 akituhumiwa kumuua Mwangosi kwa kukusudia katika tukio lilitokea kwenye kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi, mkoani hapa.
Mwangosi aliuawa Septemba 2, 2012 akiwa kwenye kazi katika ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kijijini humo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment