GEITA: Waziri Mwigulu Aweka Gwaride la Utambuzi, Amkamata Mchina Aliyemtesa Mtanzania

Nimefika Mgodi wa Nyamhuna unaodaiwa kuwa raia wa china ambao ni sehemu ya wamiliki wa mgodi huo wakishirikiana na watanzania walimtesa kinyama na kumjeruhi mmoja wa mtanzania mwenzetu aliyekuwa akifanya kazi katika mgodi huo uliopo Katoro-Geita.

Imenilazimu kufika gereza la Geita kukutana na kijana huyo ambae yupo hai tofauti na taarifa za awali kuwa alifariki.Baada ya kujiridhisha kuanzia mavazi,majeraha,picha,sura na umbo lake kuwa ndiye kijana aliyeteswa vibaya na picha zake kusambaa mitandaoni na vyombo mbalimbali vya habari,niliamua kwenda naye hadi mgodini lilipofanyika tukio hilo la kinyama,aliwatambua wahusika ambao NI KWELI WALIFANYA TUKIO HILO LA KINYAMA NA LISILOKUBALIKI HAPA NCHINI.

Hivyo walioshiriki tukio hilo tumeshawashikilia kupitia jeshi la polisi tayari kwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Nalaani tukio hilo vikali sana,serikali hii ipo tayari kushirikiana na kila mmoja rai mwema kutoa taarifa popote pale za matukio au viashiria viovu na vinavyohatarisha usalama wetu.

"Usalama wetu,jukumu letu sote"

Copy and Paste from Mwigulu Nchemba Facebook Wall

My take
Huu Unyama unaofanywa na Raia wa Kigeni hapa Nchini kwetu unatakiwa kuchukuliwa kwa hatua kama hizi tena haraka sana iwezekanavyo. Mijitu isiyokuwa na Huruma pamoja na Kumtesa kwa kumsurubu Mtanzania mwenzetu, bado haikutosheka Ikambambika kesi na kumsweka Lupango ndugu yetu huyu.

Haya hayafanywi tu huko Migodini, Hata hawa Wahindi wanawanyanyapaa sana Dada zetu wanaofanya kazi za Nyumbani kwenye Makazi yao. Serikali inapaswa kupanua jicho kuangalia wananchi wake wanavyonyanyapaliwa na hawa wageni huku wao wakiishi kama wako kwao.

Heko Mwigulu Nchemba.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment